Kwa Jibu hili la Mzee Butiku nadhani Serikali ya Rais Samia chini ya CCM isione Aibu Kukubali Katiba Mpya kwani kwa sasa haizuiliki kabisa

Kwa Jibu hili la Mzee Butiku nadhani Serikali ya Rais Samia chini ya CCM isione Aibu Kukubali Katiba Mpya kwani kwa sasa haizuiliki kabisa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Swali ( Farhia Middley dakika 45 ITV )

Je, Mzee Butiku Tume za Uchaguzi barani Afrika huwa ziko huru na kutenda Haki katika Chaguzi?

Jibu ( Mzee Joseph Butiku wa MNF )

Ni Akili ya Kawaida tu isiyohitaji Elimu Kubwa kujua ya kwamba Mkuu wa Tume ya Uchaguzi aliyeteuliwa na Rais atathubutu kwenda Kinyume na Yule aliyemteua kuwa hapo.

Kwa Uhondo Kamili wa ' Madini ' ya Mzee wangu huyu ' Genius ' kabisa kutokea ' Uzanakini ' Mkoani Mara ( Musoma ) Joseph Butiku usikose Kutizama Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV Kesho Jumatatu 31 May, 2021 Saa 3 Kamili Usiku.

Msimamo wangu GENTAMYCINE nami ( japo ni mwana CCM lia lia ) juu ya Katiba Mpya ni ule ule kuwa naitaka tena haraka mno kwani Katiba ya 1977 ina ' Vipengele ' vingi vya Kipuuzi Kipuuzi ambavyo vimepitwa na wakati na haviendani kabisa na Nyakati hii tuliyopo na hata ile ijayo.

Tafadhali wanaotokea Mikoa hii ya Kagera, Singida, Kigoma, Kondoa Dodoma na Ukerewe Mwanza wakichangia Uzi huu wawe na Adabu zote japo itapendeza zaidi kama wakiwa Watazamaji na Wasomaji ili Wasinichoshe ' Kipanga ' wa ukweli kuwahi kutokea Mkoani Mara ( Musoma )

CCM Wenzangu Katiba Mpya muhimu.
 
kuna swali aliulizwa kuhusu wabunge wa Ndugai nasubiri jibu lake kwa hamu maana huyu mzee ana uthubutu huwa haogopi
Amesema...Wabunge wa Viti Maalum au COVID 19 hawakusitahili kuwa Bungeni kwa sababu Chama chao kiliwafukuza. Akasisitiza kuwa Speaker alikosea. Amesema kuwa makosa yakifanyika huwa wanarekebishwa. Tatizo ni pale tunapoona aibu kukiri makosa husika.
 
kuna swali aliulizwa kuhusu wabunge wa Ndugai nasubiri jibu lake kwa hamu maana huyu mzee ana uthubutu huwa haogopi
Ukipata Elimu ya Ujasusi tena kutoka kwa Wenyewe Mossad hutoweza Kumuogopa Mpuuzi yoyote na daima utasimamia katika Mstari na Ukweli tu. Na sikumbuki ni Tawala gani hapa nchini ambayo kama ' ikikengeuka ' tu Mzee Butiku atanyamaza na kuacha Kukemea ( Kuonya ) hata ksma anajua ni mwana CCM Mwenzao.

Mzee Joseph Butiku na Wazee wengine Watatu ( siwataji kwa Unyeti wao na Maadili ) yao ndiyo walikuwa ' Think Tanks ' wa Hayati Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere hali inayopelekea Mzee Butiku na hao Wenzake Watatu Kuheshimika sana na Mataifa mengi ya Afrika ( hasa hasa Uganda,Rwanda, Ghana, Botswana, Mozambique, South Africa, Burundi, Misri na Algeria ) bila kusahau nchi za China, Cuba, Israel, Russia, France na England kwa nje ya Bara la Afrika.
 
Amesema...Wabunge wa Viti Maalum au COVID 19 hawakusitahili kuwa Bungeni kwa sababu Chama chao kiliwafukuza. Akasisitiza kuwa Speaker alikosea. Amesema kuwa makosa yakifanyika huwa wanarekebishwa. Tatizo ni pale tunapoona aibu kukiri makosa husika.
... umeona wapi mazungumzo wakati kipindi kwa mara ya kwanza kitarushwa kesho?
 
Ukipata Elimu ya Ujasusi tena kutoka kwa Wenyewe Mossad hutoweza Kumuogopa Mpuuzi yoyote na daima utasimamia katika Mstari na Ukweli tu. Na sikumbuki ni Tawala gani hapa nchini ambayo kama ' ikikengeuka ' tu Mzee Butiku atanyamaza na kuacha Kukemea ( Kuonya ) hata ksma anajua ni mwana CCM Mwenzao.

Mzee Joseph Butiku na Wazee wengine Watatu ( siwataji kwa Unyeti wao na Maadili ) yao ndiyo walikuwa ' Think Tanks ' wa Hayati Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere hali inayopelekea Mzee Butiku na hao Wenzake Watatu Kuheshimika sana na Mataifa mengi ya Afrika ( hasa hasa Uganda,Rwanda, Ghana, Botswana, Mozambique, South Africa, Burundi, Misri na Algeria ) bila kusahau nchi za China, Cuba, Israel, Russia, France na England kwa nje ya Bara la Afrika.
Nakumbuka 2015 karibia na uchaguzi mkuu aliwachambua wagombea bila kupepesa macho, ilikuwa kama msumari wa moto kwa baadhi yao
 
Kinacho rushwa kesho ni recorded. Radio one huwa wanatoa baadhi ya sehemu ya mahojiani hayo kuelekea siku ya kuonyeshwa kipindi Live. Sikiliza na Radio Mkuu. Usishinde jamii Forum tu...
... asante sana.
 
Back
Top Bottom