Kwa Jibu hili la Mzee Butiku nadhani Serikali ya Rais Samia chini ya CCM isione Aibu Kukubali Katiba Mpya kwani kwa sasa haizuiliki kabisa

Huyu mzee mnafiki sana!

Wakati wa utawala wa Magufuli,huyu mzee,pamoja na mapungufu ya Magufuli kwenye utawala wa sheria na udikiteta wake,alikuwa amegeuka mpiga mapambio!

Alikuwa wapi kuyasema haya? Aliwaacha kina Jenerali Ulimwengu na,angalau,Msekwa watusemee peke yao!

Huyu mzee zamani nilikuwa namheshimu sana kabila sijajua rangi yake halisi. Alipoheuka mpambe wa mtawala katili Magufuli,nikamdharau kabisa.
 
Kinacho rushwa kesho ni recorded. Radio one huwa wanatoa baadhi ya sehemu ya mahojiani hayo kuelekea siku ya kuonyeshwa kipindi Live. Sikiliza na Radio Mkuu. Usishinde jamii Forum tu...
Yaani na ITV wamekuwa wakitoa 'clip' ya mahojiano yaliyofanywa....
 
Warioba sawa. Huyo ni kiongozi mwenye principles. Mzee Butiku hapana, wakati wa dikteta,amejidhalilisha sana! Sijui alipewa nini? Au magu alikuwa anatumia charms?
 
Kama Rais hawezi kuwateua Tume kwa sababu tu ni mtu wa Chama fulani, hiyo tume iteuliwe na nani sasa? Rais hupigiwa kura na watanzania wote, kutokanana vyama vingi vikipambanishwa kwa ilani zao. Rais huyo ana madaraka ya kunyongwa mtu au kutonyongwa, anamiliki ardhi yote yaTanzania kwa niaba yetu sote. Kwa mini tusimwamini kumchagua Jaji wa Tume ambaye sifa zake zinajulikana?

Mahakama Kuu ya Marekani Supreme Court, je iko huru? Ukipeleka kesi yoyote leo, kura inajulikana fika matokeo ni 7-3 au 3-7 kutegemea itikadi yake; au hata Kenya jirani yetu mahakama kuu yake imefuta ushndi wa Kenyatta 2017 kwa misingi ya kabila, na BBI juzi hvyohivyo. Is that what we want?

Kusema kuwa mtu hana chama maana yake nini? Jenerali Ulimwengu au Fatma Karume au Askofu Bagonza for sure siyo CCM, je tuwaweke hawa wawe Tume? Penda usipende, the only alternative is tucchaguliwe na Marekani au na Kenya. Au aletwe na shetani.
 
ningefarijika mno kama huyu Mzee Butiku pamoja na hata wazee wenzake wangeyasema haya ilihali JPM akiwa hai.
 
Nawataja. Butiku. Warioba hakosi hapo. Yule mhindi hindi hivi Professor Shivji na Salim Hamed Salim. Natania tu,ila ndio ninaowaelewa
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo huru na haifuati au kupokea amri au Ushauri wa kiongozi wa Chama chochote cha siasa au Mtu yeyote kulingana na Ibara ya 74 (11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 77.
 
Sijui tu Kaijage na Mahera wanajisikiaje.
Mkuu nikiwaangalia hao watu wawili napata shida sana ya kuwatafsiri: Huyo wa kwanza ame-enjoy elimu bure na keki ya Taifa vyakutosha pamoja na mafao yakutosha, nilitegemea hange jeopardize professional yake. Huyu wa pili naye bado kijana amesahau kuwa anasafari ndefu kwenye kusimamia taaluma yake isichafuliwe. Hapo ndipo nipokata tamaa na viongozi wetu.
 
Jah People, Tale, Msukuma nawaaminia katika hili la katiba mpya.
 
Katiba iwatake vyama vya siasa kuteua mgombea Urais ambaye amekitumikia chama chake kwa muda mrefu, amepitia ngazi mbalimbali za uongozi wa chama chake na ambaye atatekeleza Sera za Chama kwa mujibu wa Katiba ya Chama chake na KATIBA ya NCHI. AIDHA Rais asiwe Mwenyekiti wa Chama wa chake cha Siasa. Vinginevyo maendeleo tutayasikia tu kwa wenzetu.
 
Mkuu LGF kama una umri mkubwa kidogo utanielewa. Chaguzi zimefanyika nyingi sana hapa Nchini. Kuanzia chaguzi za Chama kimoja mpaka vyama vingi hadi awamu ya miaka mitano ya kwanza chaguzi zote zilikuwa huru kwa asilimia 70-80. Waangalizi wa chaguzi hizo walikuwa migambo tu, na kazi yao kubwa ni kuhakikisha foleni inazingatiwa. Kipindi cha pili cha awamu ya 4 uhuru kwenye uchaguzi ulipungua na askari wakajitokeza, awamu iliyofuata mambo yalibadilika sana hadi kupelekea chaguzi kufanyika siku mbili, chaguzi za Serikali za Mitaa kutofanyika kwa mujibu wa KATIBA. Hivyo basi kutokana na hali hiyo ndipo madai ya mifumo dhabiti ya chaguzi ynapojitokeza, na mifumo hiyo lazima IWEKWE KWENYE KATIBA. NATUMAINI NIMEELEWEKA
 
Na itapendeza zaidi vyama vya siasa kuwa na mchakato huru utakaosimamiwa na kamati huru ktk chaguzi za ndani ya chama ili watuletee wagombea wenye weled na watakaopatikana kidemokrasia kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama husika.
 
Yawezekana ana hoja ya maana lakini mbona hatukumsikia wakati wa Mwendazake akizitoa hoja hizo kwa wananchi? Nina wasiwasi sana na malengo hasa ya hawa wazee wetu.
 
Aanze na mabadiriko kwenye Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwanza, huyu na Warioba wanapenda sifa na legacy ambazo kamwe hawawezi kuwa nazo, kutwa kwenye midahalo na vyombo vya habari, sijui watastaafu lini, kuna maisha nje ya porojo za kisiasa. warudi vijijini wakachunge mbuzi na wajukuu zao,mawazo yao yamepitwa na wakati.
 
Uzi mzuri ila pale tu ulichoniudhi ni kusema watu kutoka mkoa wangu wasichangie,wakati mkoa ninaotoka una bahati ya kuwa na binadamu mwenye akili nyingi kupita kiasi ndio nachoka kabisa ☹️☹️☹️
Kama huamini muulize polepole alikuwa na wasanii 200 jukwaani lakini raia hawaelewi ila mwamba anatembea na flash moja wimbo mmoja kamfanya hadi mwenzake kafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…