Kwa Jinsi 'Kiboko ya Wachawi' anavyowadhihaki Watanzania, ipo haja ya mamlaka inayosajili makanisa na taasisi nchini kuongeza umakini

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,089
Reaction score
9,664
Katika Siku za Karibuni zimeonekana 'Klipu' kadhaa Za Mchungaji anayejiita Kiboko ya wachawi mitandaoni zikimuonyesha akiwadhihaki na kuwadhalilisha Waamini waliokuwa wakitoa pesa zao kwake kwa madhumuni ya kuombewa. Ameonekana akisema 'amezimiss' Laki tano tano.

Ingawa wapo watakaosema kuwa wahanga walijitakia wenyewe, lakini tukumbuke wahanga hao ni watu waliokuwa na matatizo walienda kule wakiwa na matumaini ya kupata msaada (yaani watu desperate), badala yake wamekutana na madhira hayo.

Pia, soma: Kiboko ya Wachawi aonekana DR Congo, awatambishia Watanzania kuwa anakula maisha. Asema amemisi zile laki tano za kiingilio

Watu wengi huwa wanapoteza pesa zao, Lakini kitendo cha mtu kuanza kurusha klipu mara yupo supermarket anatanua na pesa za wahanga, mara anasema anamiss laki tano tano za waTZ, mara akejeli kwamba mtu asimkabili yeye kwanza akajenge nyumba ya baba yake na kejeli lukuki sio poa kabisa.

Kulifungia hilo kanisa ilikuwa ni hatua ambayo ilikuwa haiepukiki, lakini ipo haja ya Wenye Mamlaka ya Usajili wa Taasisi na Makanisa kuongeza umakini katika hilo, la sivyo matapeli wataendelea kutumia mlango huo.
 
Makanisa yenye manabii matapeli tu

Ova
 
Msajili wa makanisa na yeye ni binadamu, yaani aachie dola 10,000 kusajili kanisa lolote lililoleta maombi nchini.
 
😂 kwahiyo kwa utovu wenu nyie mnaomba msaada kama alisajiri na akafata vigezo vyote kwanini asipewe vibali..?
mmeliwa mmeliwa tu kila siku tunapigana kelele humu jukwaani ni uhuni tu hamsikiii tulieni dawa iwaingie na najua hapo bado mpk damu imwagike sana ndo mtaelewa.
 
aliwaambia dini,imani zinatibu matatizo ni nani..? zimekuwepo tokea zamani na matatizo yapo palepale tukiwaambia hivyo vitabu vyenu vya dini havina maana hamuelewi vinamakosa lukuki hamsikii,watu wanashikwa akili kijinga mno! kazeni mishipa ikibidi namimi ntakuwa nabii ili nije nijizolee dolari
 
Katika Siku za Karibuni zimeonekana 'Klipu' kadhaa Za Mchungaji anayejiita Kiboko ya wachawi mitandaoni zikimuonyesha akiwadhihaki na kuwadhalilisha Waamini waliokuwa wakitoa pesa zao kwake kwa madhumuni ya kuombewa. Ameonekana akisema 'amezimiss' Laki tano tano.

Ingawa wapo watakaosema kuwa wahanga walijitakia wenyewe, lakini tukumbuke wahanga hao ni watu waliokuwa na matatizo walienda kule wakiwa na matumaini ya kupata msaada (yaani watu desperate), badala yake wamekutana na madhira hayo.

Pia, soma: Kiboko ya Wachawi aonekana DR Congo, awatambishia Watanzania kuwa anakula maisha. Asema amemisi zile laki tano za kiingilio

Watu wengi huwa wanapoteza pesa zao, Lakini kitendo cha mtu kuanza kurusha klipu mara yupo supermarket anatanua na pesa za wahanga, mara anasema anamiss laki tano tano za waTZ, mara akejeli kwamba mtu asimkabili yeye kwanza akajenge nyumba ya baba yake na kejeli lukuki sio poa kabisa.

Kulifungia hilo kanisa ilikuwa ni hatua ambayo ilikuwa haiepukiki, lakini ipo haja ya Wenye Mamlaka ya Usajili wa Taasis na Makanisa kuongeza umakini katika hilo, la sivyo matapeli wataendelea kutumia mlango huo.
Na ndio maana nimeamua kubaki hapa parokiani kwangu kwenye hiki Kigango Cha Mt. Anthony wa Padua
 
Ingekuwa teeth ni Kama mossad tungemfuata hukohuko, tungemsaforisha ndani ya begi, angejikuta yupo chato, tungemkamua hizo laki tano zingemtokea popote penye nafasi
 
aliwaambia dini,imani zinatibu matatizo ni nani..? zimekuwepo tokea zamani na matatizo yapo palepale tukiwaambia hivyo vitabu vyenu vya dini havina maana hamuelewi vinamakosa lukuki hamsikii,watu wanashikwa akili kijinga mno! kazeni mishipa ikibidi namimi ntakuwa nabii ili nije nijizolee dolari
Hapa Tanzania we jiite nabii tu. Utajiri utaukimbia mwenyewe😂😂😂
 
Katika Siku za Karibuni zimeonekana 'Klipu' kadhaa Za Mchungaji anayejiita Kiboko ya wachawi mitandaoni zikimuonyesha akiwadhihaki na kuwadhalilisha Waamini waliokuwa wakitoa pesa zao kwake kwa madhumuni ya kuombewa. Ameonekana akisema 'amezimiss' Laki tano tano.

Ingawa wapo watakaosema kuwa wahanga walijitakia wenyewe, lakini tukumbuke wahanga hao ni watu waliokuwa na matatizo walienda kule wakiwa na matumaini ya kupata msaada (yaani watu desperate), badala yake wamekutana na madhira hayo.

Pia, soma: Kiboko ya Wachawi aonekana DR Congo, awatambishia Watanzania kuwa anakula maisha. Asema amemisi zile laki tano za kiingilio

Watu wengi huwa wanapoteza pesa zao, Lakini kitendo cha mtu kuanza kurusha klipu mara yupo supermarket anatanua na pesa za wahanga, mara anasema anamiss laki tano tano za waTZ, mara akejeli kwamba mtu asimkabili yeye kwanza akajenge nyumba ya baba yake na kejeli lukuki sio poa kabisa.

Kulifungia hilo kanisa ilikuwa ni hatua ambayo ilikuwa haiepukiki, lakini ipo haja ya Wenye Mamlaka ya Usajili wa Taasis na Makanisa kuongeza umakini katika hilo, la sivyo matapeli wataendelea kutumia mlango huo.
Kwanza ni sawa tu kawanyoosha hivi mtu na akili yako umezaliwa umekuta wazazi wako wanaabudu imani flan au dhehebu flan leo hii umekuwa unatafuta madhehebu yako tena unaambiwa lipia na unalipia wakati ulipokuwa mdogo hujawahi sikia lipia ili uombewe. Wacha wanyoonywe mpaka watie akili kichwani. Tena jamaa angewapururua vya kutosha. Mtu toka asubuhi unashinda unalia tu hutafuti pesa upo kwa nabii feki hata mme wako humkumbuki sasa huo si wehu.Jamaa sawa sawa kawanyuka na utashangaa ataibuka mwingine na bado watapigwa tena
 
Hakuna haja ya kuisumbua serikali, leo serikali ya samia ikisema ichukue hatua dhidi ya udanganyifu, hata hao waliobaki wataondolewa, ndipo mtaamka tena kusema serikali inaingilia uhuru wa kuabudu, eg Mh kagame anapakwa matope yakutosha kwa uamuzi wa kufunga makanisa ya kitapeli. Serikali haiwezi kuja kukaa mlangoni kwako ikuzuie, nyie nendeni mkatoe sadaka hadi nyumba zenu, wajinga ndio waliwao.
 
Anafanya Vizuri,labda maana anaboost bongo lala za watanzania..........acha aendelee kutoa somo
 
Back
Top Bottom