Kwa kauli hii, CCM yafaa ifutwe kwa kutoiheshimu Katiba

Kwa kauli hii, CCM yafaa ifutwe kwa kutoiheshimu Katiba

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Katika hali ya kuonyesha kuwa uongozi wa CCM hauheshimu Katiba wala Utawala wa sheria, umetoa ifuatayo kama taarifa rasmi ya vikao vyake vya Dodoma:-
Kwa kutambua kuwepo matatizo ya matamshi na vitendo visivyoridhisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi, Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kuunda Kamati Ndogo ya kutafuta undani wa matatizo hayo na kupendekeza kwa Kamati Kuu njia za kuyatatua. Aidha, Kamati hiyo pia itaangalia utendaji kazi wa Kamati za Chama katika Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa nia ya kubaini upungufu uliopo ili kupendekeza kwa Kamati Kuu kuhusu njia za kurekebisha. Pia, Kamati itaangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge na Baraza la Wawakilishi na kushauri namna ya kuimarisha, pale panapostahili.

Kamati hiyo itaongozwa na Mzee Alli Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Wajumbe wengine ni Mzee Pius Msekwa Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) na Ndugu Abdulhaman Kinana
.
Katiba ya Tanzania inatambua Serikali, Bunge na Mahakama kama mihimili mikuu ya dola na kulipa Bunge madaraka kwa niaba ya wananchi wote kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

Katiba inaendelea vile vile kumlazimisha Mbunge kula kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge. Katiba hiyo hiyo inatoa uhuru kwa mawazo, majadiliano na utaratibu katika bunge na huo uhuru hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali pengine popote nje ya Bunge.

Ni katiba ndio imewezesha uwepo wa CCM na vyama vingine vya siasa na pamoja na CCM kuwa na utaratibu wake wa kichama, kama itatokea taratibu hizo zikapingana na katiba, zinakuwa batili. CCM kama hairidhiki na uendeshaji ndani ya Bunge inaweza kuitumia kamati ya wabunge wa CCM kuwasilisha hoja bungeni.

Kwa CCM kuunda kamati nje ya Bunge eti kuangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge, imezidi kukiuka katiba ya nchi na adhabu yake ni kupoteza sifa kama chama cha siasa kulingana na sheria kama zilivyotungwa na bunge hilo hilo na yafaa ifutwe kwenye daftari la msajili wa vyama.

Kamati ya Mwinyi Rais Mstaafu, Msekwa Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) na Ndugu Abdulhaman Kinana kama zitatekeleza majukumu waliyopewa watakuwa wanafanya makosa ya jinai - waitwe na wahojiwe na Bunge. Taifa haliwezi kuendelea kuongozwa kihuni bila kufuata sheria na taratibu kama katiba inavyoagiza.
 
Mkuu CCM sasa ni sawa na mlevi wa mnazi, anajinyea tu!
 
Mkuu Mag3,
Sioni kama kamati hiyo itaingilia chochote juu ya Bunge na B'la wawakilishi.
 
Mag3 said:
........Pia, Kamati itaangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge na Baraza la Wawakilishi na kushauri namna ya kuimarisha, pale panapostahili.


Mkuu Mag3,
Sioni kama kamati hiyo itaingilia chochote juu ya Bunge na B'la wawakilishi.

Kama ni hivyo, basi kamati hiyo haitafanya kazi yo yote au kazi kamili iliyoteuliwa kufanya.....
 
Mkuu Mag3,
Sioni kama kamati hiyo itaingilia chochote juu ya Bunge na B'la wawakilishi.
Mkuu Kibunango, unaelewa nini na hili ambalo limetolewa kama tamko rasmi la CCM kwenye website yao:-
Pia, Kamati itaangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge na Baraza la Wawakilishi na kushauri namna ya kuimarisha, pale panapostahili.
Ninavyoelewa mimi Kamati itachunguza na kupendekeza kwa Kamati Kuu ya CCM hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo isiyoridhisha ( kwa maoni ya CCM ) ya uendeshaji wa Bunge. Je, wewe unaelewa nini ndugu yangu Kibunango ?
 
Naona inawalenga wabunge na wawakilishi wa CCM kwenye vyombo hivyo pasipo kuingilia shughuli za vyombo hivyo.

Lengo ni kuona kuwa chama kinakuwa na msimamo wa pamoja huko kwenye utungaji wa sheria na mikakati ya pamoja ili kukifanya chama kuwa na nguvu ya kweli kulingana na idadi ya wabunge/wawakilishi wake.
 
CCM sio ifutwe ni chama ambacho kilihitajiwa kuvunjwa pale tu kulipoanzishwa sheria ya vyama vingi.CCM isingeliruhusiwa kuendelea kwani ni Chama ambacho kimetokea kuwa cha WaTanzania wote hapo kabla na hivyo uhalali wake wa kuwepo kama Chama katika mfumo wa vyama vingi utakuwa na utata ,na ukiangalia utaona imejikita katika sehemu zote kuu ,hivyo haiwezekani Chama hiki kuwa katika mizani moja na vyama vingine na ndio ukaona kuwa kila pembe huwa kina nguvu ndani ya vyombo vya serikali na nje ya serikali ndani ya nchi na nje ya nchi ,mali zote za nchi zipo chini ya chama hiki ,imehodhi mambo yote.Na sasa wanakwiba.
 
Huko kwiba ni kwa kila mtu. Hata hao wapinzani wakipata watakwiba tu. In fact wao ndio watakwiba zaidi. Dawa ni kila mwizi kupigwa risasi tu!
 
Back
Top Bottom