Kwa kauli hii ya Mbowe, Katiba si muhimu sana bali tuombe Tanzania isimpate Rais Katili na Mwendawazimu

Kwa kauli hii ya Mbowe, Katiba si muhimu sana bali tuombe Tanzania isimpate Rais Katili na Mwendawazimu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Kwa Madaraka makubwa aliyonayo Rais kutokana na Katiba iliyopo akiwa ni Rais mzuri haina shida, ila akiwa ni Rais Katili au Chizi anaweza kuipeleka nchi kubaya sana "

Chanzo: BBC Dira ya Dunia Leo hii.

Haya mnaoshupalia Katiba mpya na kutupigia Kelele zenu za 'Nongwa' kila Siku Mh. Mbowe hana shida nayo sana ila mkazo wake mkubwa tu ni Rais wa Tanzania asiwe ni Katili na mwenye Uchizi (Uwendawazimu).

Hivyo basi nami GENTAMYCINE nahitimisha kwa kuwaomba kuanzia sasa tuachaneni na kudai Katiba Mpya na tujikite hasa katika Kumuomba Mwenyezi Mungu awe anatupa Marais wazuri, wema, wachapakazi na wasio Makatili na Wendawazimu kama Hayati Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa, Mzee Kikwete, Hayati Dkt. Magufuli na Mama yetu Rais Samia.

Asante sana Mheshimiwa Freema Alkaeli Mbowe kwa Kulihitimisha hili vyema kabisa na ni Matumaini yangu sasa Makelele ya Kudai Katiba mpya nchini Tanzania yatapungua kama si Kuisha kabisa ili Watanzania tuendelee Kuchapa kazi ya Kujenga nchi yetu kwa Katiba yetu hii hi ya mwaka 1977 ambayo kwa bahati nzuri haijawahi kutuletea Tanzania Marais Makatili na Machizi (Wendawazimu) tokea Historia ya Uhuru wa Taifa hili.
 
Katiba ya sasa siyo tatizo la kwanza, ila tatizo lililopo kwa Watanzania wengi ni kukosa utamaduni wa kuheshimu katiba na sheria zake.

Lazima tuanze kujenga utamaduni tangu utotoni kutii sheria bila shuruti.

Tujiulize, mbona Watanzania wengine hawaiheshimu hata hiyo katiba ya 1977?

Mbona Watanzania hatujitokezi kuilinda hiyo katiba ya 1977 inapovunjwa? Je, tukipata katiba mpya si yatakuwa yaleyale?

Ikitokea tumeipata katiba mpya, na mtu fulani akaivunja, je tupo tayari kumpinga kwa nguvu zote, ikiwemo kuandamana?

Tazama Watanzania tunavyovunja sheria, si viongozi wala wananchi, wote ni kuvunja sheria. Mfano mdogo tu, wangapi humu wana magari na hawajakata bima wala leseni? Wakikamatwa wanawapa Polisi rushwa, na Polisi anachukua rushwa wakati anajua ni kosa!
 
IMG_20210510_004157.jpg
 
Back
Top Bottom