Savimbi Jr
JF-Expert Member
- Sep 23, 2011
- 6,818
- 9,183
Hawatendei haki watumishi wa UMMA yaani ana character za umungu "MTU".Huyu mzee aache upumbavu standing orders za utumishi wa umma ziko wazi, mtu anayetaka kuomba nafasi ya kisiasa huwa anapewa ruhusa ya bila malipo mpaka mchakato utakapoisha. Akipewa ridhaa ya kukiwakilisha chama ndiyo utumishi wake unakomea hapo! Aache unyanyasaji huyu
Hivi yeye angeridhika na alichonacho,leo angekuwa Rais ?Come on !Aluposema watu waridhike na walicho nacho. Walioteuliwa na wanajitoa ili wagombee watakatwa
Hivi yeye angeridhika na alichonacho,leo angekuwa Rais ?Come on !
Nadharia hiyo ndiyo inawafanya watu wapagawe,pia vinono vilivyopo Bungeni unajipakulia upendavyo.Watanzania wanyonge wawakilishi wao wanaishi kifalme na hakuna wa kuwadhibiti.Ni nadharia rahisi kuielewa.
Tofauti na awamu zilizopita, kuwa mteule wa Rais kwenye awamu hii ni sawa sawa na kukalia kuti kavu, ni stress na huna uhakika kama utabaki salama, lolote laweza kutokea, mfanya maamuzi ni mtu mmoja, inategemea anavyojisikia, anaweza kuamka ukasikia ametengua nafasi yako, hivyo wateule wanaomalizia kipindi hiki wameshaling'amua hilo na limewatesa sana. Lakini kuwa mbunge ni tofauti, unakuwa umechaguliwa kwa nguvu ya wananchi wengi, maamuzi ya wengi, na si ya mtu mmoja, inakupa uhakika wa kuwa mjengoni kwa miaka mitano na hata mfanya uteuzi akikuona anaweza kukuteua kuwa waziri au nafasi yoyote kubwa, na hata ikitokea ukatumbuliwa nafasi ya uteuzi mf, uwaziri, bado unabaki na ubunge wako kwa miaka mitato, nani anataka stress?
Hilo la Mbowe na CHADEMA unalijua wewe, mimi nimeliandika la CCM.chadema ni Mali ya Mbowe kama saccos akiamua lolote kaamua tu