Nawasalimu kwa jina la Jamhuri. Nimekuwa nikifuatilia kauli mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa dhidi ya hayati Magufuli. Ni wazi kabisa kuna chuki kubwa dhibi yake. Na ukichunguza kwa undani zaidi utaona wanataka kupandikiza hiyo chuki hata kwa wananchi wa kawaida.
Ukweli ni kwamba wananchi wengi wa kawaida hawawezi mchukia magufuli, utamchukiaje kiongozi aliyejenga zahanati nchi nzima? Shule, madaraja, Barabara? Viwanja vya ndege? Shule? Miradi mikubwa ya umeme? Kujenga makao makuu ya Dodoma kwa kiwango kile tena kwa muda mfupi? Treni ya mwendo kasi?
Kichaa anawezaje kufanya yote haya? Haya tuonyesheni hao wengine wamefanya nini katika miaka 10?
Ujambazi, mauaji ya albino yaliisha, umeme kukatika kulikoma, kichaa anawezaje kufanya yote haya?
Mungu atatuhukumu siku moja, na hakika tutahukumiwa kwa matendo yetu.
Lazima Magufuli achukiwe na matajiri na wanasiasa. Utawezaje tetea masikini huku ukifurahisha matajiri? Haipo hata siku moja.
Ukiniuliza leo viongozi waliolifanyia makubwa taifa hili toka liwepo list yangu iko hivi
1. Julius Nyerere
2. John P. Magufuli
3. Benjamin Mkapa
4. Ally Hassan Mwinyi
5 Jakaya Kikwete
Mama Samia sijamuweka sababu bado yupo madarakani. Anaweza kuwa wa Kwanza au wa mwisho inategemea atalifanyia nini taifa hili.
Mungu ibariki Tanzania.