Namichiga
JF-Expert Member
- Jun 1, 2017
- 356
- 526
Ndugu wana jukwaa, kwenye kichwa cha habari hilo ni swali, hivyo katika kutoa hoja naomba kwanza tutangulize kwanza kujibu na baadae ndio zifuatie hoja za uchambuzi.
Katika maswala mazima ya mifumo ya kiutawala katika nchi za Kiafrika, hili neno la propanda linapewa kipaumbele kikubwa pindi inapojitokeza mihemko ya jamii ya watawaliwa, na idara maalum zinazohusika na mipango hii ya propaganda hukaa chini na kuibua jambo litakalokuwa midomoni mwa wananchi na kwenye vyombo vyote vya habari kwa wakati huo, dhamira kuu ni kuiacha serikali ipumue dhidi ya masimango na maneno kutoka kwenye jamii kwa wakati huo!
Nije kwenye kiini cha mada,kwa mtazamo wangu mimi, hili swala la serikali kumtia nguvuni mwenyekiti wa Chadema Bw. Mbowe na kumpandisha kizimbani na watuhumiwa wengine katika makosa ya ugaidi, serikali kwa ujumla imejaribu kuhamisha goli ili wanaoshambulia wakose muelekeo.
Sote tunajua, baada ya kukamata usukani wa madaraka Rais Samia, kipaumbele chake chake cha kwanza mkononi kilikua ni kuirudisha Tanzania kwenye nafasi yake katika ramani ya Kidemokrasia ulimwenguni.Na matamshi yake akauthibitishia ulimwengu kwamba yale mambo yote yasiyokuwa ya kiungwana katika utawala wake hayatakuwepo.
Hapa sasa,kiujumla hadi mwenda zake anatangulia mbele ya haki, uwanja wa demokrasia nchini ulishajaa tope na vyama vya upinzani vilikua hoi bin taabani.Miongoni mwetu watanzania wa kawaida hakuna asie fahamu hilo.
Hivyo basi upinzani upinzani ukajaribu kusuka ajenda kuu itayowapa kick ili kutembelea nyota ya Samia na kurudisha umaruufu wao uliopokonywa kwa mabavu, na katika kuzichanga karata zao wakaona ajenda namba moja ni katiba mpya.
Wakaanza kuliamsha dude nchi nzima tena kwa spidi kubwa huku wakijaribu kuwatumia hadi watu mbalimbali wenye ushawishi kwa jamii ili kupata attention. Na serikali kadri ilivyojaribu kutumia maneno ya hekima na busara ili waachane na jambo hilo,ndio kwanza wakazidi kupata kick.
Hapo ndio serikali ikaamua kuwakabidhi jukumu watu wa kitengo ili kuhamisha goli la mjadala huo waliokuwa nao wapinzani.
Na watu wakainama, wakainuka na wakaamua kufukua makaburi kwa kuirudisha tena ubaoni kesi ya ugaidi ambayo kwa maneno ya ndani inasemekana, walishaichumbua na kujiridhisha kwamba haina ukweli.
Na baada ya Bw. Mbowe kupandishwa kizimbani hatimaye lengo lao limetimia kwani upande wote wa upinzani umeshatawanyika na wanahaha na kesi ya mwenyekiti.