Kwa kesi hii ya ugaidi ya akina Mbowe: Je, Kitengo cha propaganda ndani ya Serikali wamefaulu au wamefeli?

Kumbe kazi ya TISS ni kufanya Propaganda? Yawezekana basi hata CIA nao kazi yao Kubwa huko Marekani ni Kufanya tu Propaganda.

Kazi kweli kweli.....!!
Kumbe hujui kazi ya CIA, umesahau propaganda za Sadamu kumiliki WMD zilienezwa na nani.
 
Kumbe hii nayo ilikuwa propaganda??
 
mi nasemaga Raisi pekee aliyeweza kumudu siasa za ushindani ni JK hawa wengine wanachojua ni kutumia dola sasa tatizo nyakati zinabadilika saahivi kuna mtandao watu wanapata na kutoa taarifa kwa haraka na kwa wepesi sana, matokeo take ndio hivi kuvuliwa shungi mbele ya mkweo
 
Lowasa anakuja chadema ni asset au liability ....hapo ndipo aliamua kusimamia analolijua Hadi Leo kwakweli mhuuuu
Ukweli mchungu ni kwamba kwa wagombea urais from opposition tokea mfumo wa vyama vingi uanze kuna aliyewahi kupata kura nyingi na wabunge wengi kumzidi Lowasa??
 
Kumbe hujui kazi ya CIA, umesahau propaganda za Sadamu kumiliki WMD zilienezwa na nani.
Kwahiyo kazi ya CIA ni kufanya Propaganda? Kazi kweli kweli na sasa naamini Elimu ya Tanzania ipo ICU.
 
Hoja ya bandiko lako ni nini? Bandiko hili halieleweki unachotaka tukijadili, andika upya labda utapatia.
 
Kesi ya Mbowe ipo toka mwaka jana. Leta mada nyingine.
 
Na baada ya Bw. Mbowe kupandishwa kizimbani hatimaye lengo lao limetimia kwani upande wote wa upinzani umeshatawanyika na wanahaha na kesi ya mwenyekiti.
Punguza mihemko dada yangu utatafikiri unaingia 'leber' kwa mara ya kwanza.
 
Propaganda zingine humaliza na kuwaabisha wapishi wake kama hii dhidi ya mbowe
 
Kumbe kazi ya TISS ni kufanya Propaganda? Yawezekana basi hata CIA nao kazi yao Kubwa huko Marekani ni Kufanya tu Propaganda.

Kazi kweli kweli.....!!
Kiongozi GENTAMYCINE,kwa nchi za kiafrika idara za usalama ndio nguzo kuu za watawala,kwa yale mema na hata mabaya.Je unafahamu kwamba nyuma ya pazia wengi waliopangwa kusimamia kesi hii kuanzia mahakamani hadi upande wa mashtaka ni watu wa kitengo?.
 
Kumbe hii nayo ilikuwa propaganda??
Ndio kiongozi,watu wa ndani kabisa wa serikali walikua wanafahamu kwamba kikombe cha babu hakina nguvu wala uwezo wowote wa kuponya maradhi sugu ya wananchi.Lakini kwa kuwa ulikuwa mpango mkakati basi ndio kwanza waliongoza misafara kwenda Loliondo!!.Lakini matokeo tuliyaona.
 
Propaganda hazijawahi kufanikiwa zaidi ya kuivuruga Taifa. Ndicho kina chotokea katika kesi hii ya hovyo kuwahi kutokea Tanzania. Ni aibu, ni aibu na ni aibu sana kwa Mama Samia na Serikali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…