Kwa kiasi hiki cha laki nne na nusu naweza fanya ishu gani hapa mjini?

Kwa kiasi hiki cha laki nne na nusu naweza fanya ishu gani hapa mjini?

KIATUE

Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
13
Reaction score
0
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi mbungani mwanza nina kiasi cha shilingi laki nne na nusu sasa naomba wana JF mnipe mawazo kitu hata kama ni chA kawaida nawezaje zalisha na kuanzisha kibiashara gani kwa kiasi hiki?
 
Siyaelewi vizuri mazingira ya mwanza ,ngoja waje ni wazo zuri kuliko kuhonga bure
 
Kwa hicho kiasi mkuu mhh ngoja waje wataalamu wa kudadavua
 
Fungua banda la chips eneo lenye mzunguko mkubwa wa watu uweke kijana baadae uza na misosi mtaji ukiongezeka
 
Tuwasiliane unipe hiyo hela niiweke kwenye biashara yangu. Halafu niwe nakupa efu 50 kila mwisho wa mwezi na pesa yako ipo pale pale. Siku ukihitaji nakurudishia.
ni pm tafadhali
 
tembelea wachomachips na mahoteli.wachoma chips wana nunuayai moja la kienyeji kwa 300 na kama utakuwaunauza kwa walaji moja kwa moj ni sh 400,ukienda minadaji vijijini yai moja ni sh100,kuna jamaa kapata kahoteli ambako wanatumia trei 10 mpaka 15 kwa ck.wanachotaka wao ni uhakika wa kupata mzigo.JICHANGANYE UPATE DETAILS MKUU.
 
:drum:...mawazo mazuri ila mazingira ya sasa labda biashara ya chakula
 
fuga kuku,anza na kuku 25@10,000=250,000. Majogoo 5,majike 20. Hiyo chenji iliyobaki itumike kwa chakula cha kuku,ujenzi wa banda kubwa na bora. Zingatia utaalam wa ufugaji. Baada ya miezi sita utaanza kuona mafanikio.
 
Tuwasiliane unipe hiyo hela niiweke kwenye biashara yangu. Halafu niwe nakupa efu 50 kila mwisho wa mwezi na pesa yako ipo pale pale. Siku ukihitaji nakurudishia.
ni pm tafadhali

Una uhakika na unachokisema?
 
Back
Top Bottom