Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi mbungani mwanza nina kiasi cha shilingi laki nne na nusu sasa naomba wana JF mnipe mawazo kitu hata kama ni chA kawaida nawezaje zalisha na kuanzisha kibiashara gani kwa kiasi hiki?
Tuwasiliane unipe hiyo hela niiweke kwenye biashara yangu. Halafu niwe nakupa efu 50 kila mwisho wa mwezi na pesa yako ipo pale pale. Siku ukihitaji nakurudishia. ni pm tafadhali
tembelea wachomachips na mahoteli.wachoma chips wana nunuayai moja la kienyeji kwa 300 na kama utakuwaunauza kwa walaji moja kwa moj ni sh 400,ukienda minadaji vijijini yai moja ni sh100,kuna jamaa kapata kahoteli ambako wanatumia trei 10 mpaka 15 kwa ck.wanachotaka wao ni uhakika wa kupata mzigo.JICHANGANYE UPATE DETAILS MKUU.
fuga kuku,anza na kuku 25@10,000=250,000. Majogoo 5,majike 20. Hiyo chenji iliyobaki itumike kwa chakula cha kuku,ujenzi wa banda kubwa na bora. Zingatia utaalam wa ufugaji. Baada ya miezi sita utaanza kuona mafanikio.
Tuwasiliane unipe hiyo hela niiweke kwenye biashara yangu. Halafu niwe nakupa efu 50 kila mwisho wa mwezi na pesa yako ipo pale pale. Siku ukihitaji nakurudishia. ni pm tafadhali