Kwa kigezo cha uhitaji wa mchezaji mzoefu wa kimataifa, kwa Larry Bwalya Simba SC tumekosea

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Habari wanajamvi na mashabiki wenzangu wa Simba SC.

Kwa nini msimu huu nimejawa zaidi na wasiwasi kuhusu usajili kuliko kawaida. Kilichonihtua hasa ni usajili mpya wa kiungo mkabaji kijana Larry Bwalya. Hivi ni kweli tumemuacha Shaiboub kwa ajili ya kijana asiye na experience kwenye medani za mitanange ya kimataifa?

Napata hata wasi wasi kuamini kwamba tumewapokonya Yanga SC huyu mchezaji. Sidhani kama Yanga SC wangevutiwa na takwimu za huyu mchezaji zaidi na takwimu za Shiboub linapokuja suala la uzoefu wa kimataifa.

Naombeni viongozi wangu wa Simba SC mnijibu, ni kweli tumewapola Yanga huyu mchezaji au mmetuhadaa sisi mashabiki?

Nasikia Yanga SC wako kwenye mazungumzo na Sharafeldin Shaiboub Ali . Kama wakifanikiwa kumsajili roho itaniuma sana. Kwa maana wao kuachana na Tshishimbi na kumchukua Shaiboub ni mafanikio makubwa kikosini kuliko sisi kuachana na Shaiboub kumchukua Larry Bwalya.

Takwimu za mechi za Sharafeldin Shaiboub Ali za kimataifa ukiachana na zile alizocheza akiwa Simba SC.


Takwimu za mechi za Larry Bwalya za kimataifa akiwa Zanaco FC mpaka alipojiunga Power Dynamos fC.


NB: Tunasajili kujiandaa au tunasajili kwa mihemko?
 
Simba walidanganywa kwamba Yanga iinamsajili Larry wakaamua kuikomoa Yanga kama kawaida yao
 
Simba walidanganywa kwamba Yanga iinamsajili Larry wakaamua kuikomoa Yanga kama kawaida yao
Jipe moyo ifikie mshali utopolo muwe wapole mjifunze kwa shabiki lialia shadeee
 
We Jamaa huwa unafurahisha sana.

Shiboub si alikuwepo hapa na kashindwa kupata nafasi na kocha hamuhitaji?

Unamzungumzia Lary ambaye Sven alikuwa akimhusudu timu ya Taifa na ndiye aliyemwita kwa Mara ya kwaza.

#mkizubaa tutawapora wachezaji wote tumgawie Biashara United.
 
Toa fedha tukasajili unaowaona wanafaa wewe bila kuzingatia maoni ya technical bench.

Kama kweli tuna weledi wa kuzingatia technical bench basi Senzo asingetukimbia, Simba tulianza vizuri lakini sasa tunaanza kupoteza uelekeo.
 
We Jamaa huwa unafurahisha sana.
Shiboub si alikuwepo hapa na kashindwa kupata nafasi na kocha hamuhitaji?
Unamzungumzia Lary ambaye Sven alikuwa akimhusudu timu ya Taifa na ndiye aliyemwita kwa Mara ya kwaza....
Unadhani kwanini wacongo na waarabu walituchezeshea viganja?

ni kwasababu waana wachezaji wengi wenye uzoefu wa mashindano makubwa.

Tulihitaji kusajili mchezaji wa kuingia kikosini moja kwa moja. huyo Larry atamuweka nani bench na uzoefu wake duni wa michuano ya kimataifa?
 
Simba walidanganywa kwamba Yanga iinamsajili Larry wakaamua kuikomoa Yanga kama kawaida yao

Hata mimi nimepata wasi wasi mtani. Ninajua kuwa yule si mchezaji wa kumzidi uwezi Shaiboub ili waliinizia mada ya kuwapora Yanga SC ili sisi mashabiki tusihoji uwezo wake tubaki kuzungumzia kuwapora Yanga SC.
 
Hivi matokeo ya AZAM FA mechi iliishaje?Tuanze na hapo. Utopolo wanapata tabu mpaka wamekuwa washauri wa Another Level. Wanatia huruma. Ukisoma twitter ya Hersi utamuonea huruma. Kachokaa.
 
Larry Bwalya kahojiwa na Mwanaspoti anadai Utopolo walitaka wamlipe kwa mafungu. Upigaji huo ndio uliomkimbiza Tshishimbi.
Usajili wa mali kauli.Imekuwa mizigo ya soko la Kariakoo?
 
demigod Nikusahihishe kidogo huyo mchezaji sio kiungo mkabaji Bali Ni kiungo mbunifu.Tukija kwenye issue ya shiboub na Larry bwalya nakuunga mkono shiboub Ni better than Larry shiboub anakuoffer vitu vingi ikiwemo ana physical ability nzuri, pia anauwezo wa kukaba than Larry, anafunga magoals than Larry, technical ability yake Ni nzuri Sana than Larry.

Kingine nilichoona ni kwamba Simba walikuwa hawajui kumtumia vizuri shiboub, Shiboub alikuwa anatumika kwenye midfielder ya chini wakati naturally yeye Ni advance midfielder.
 
Mchezaji panga pangua chipolopolo unahoji?

Squad depth inahitajika kucheza champions league.

Msimu uliopita kukosekana kwa Chama timu ilikuwa haitengenezi nafasi tena, Dawa yake ni hii hapa. Utachezaje champions league ukiwa una kikosi finyu?
 
Kama kweli tuna weledi wa kuzingatia technical bench basi Senzo asingetukimbia, Simba tulianza vizuri lakini sasa tunaanza kupoteza uelekeo.
Wewe ni mwanachama au shabiki wa club ya Simba?
 
Shiboub haendani na mfumo wa mwalimu Sven ndo maana hata benchi alikuwa hakai.....
Sio tumeshindwa kumtumia yeye ndo kashindwa kubadilika.
 
Larry Bwalya kahojiwa na Mwanaspoti anadai Utopolo walitaka wamlipe kwa mafungu. Upigaji huo ndio uliomkimbiza Tshishimbi.
Usajili wa mali kauli.Imekuwa mizigo ya soko la Kariakoo?
Magazeti sio source ya kuaminika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…