Kwa kilichotokea tutarajie Spika mpya kuwa na hofu, asiye na maajabu

Kwa kilichotokea tutarajie Spika mpya kuwa na hofu, asiye na maajabu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Wote tumeshuhudia yaliyotukia.
Yanastaajabisha na hata hivyo yanadhihirisha nyufa za wazi ambazo Kama taifa tunapaswa kuzifanyia mpango tuzizibe.

Kilichotokea kinatukumbusha umuhimu wa Katiba mpya ndani ya taifa letu.

Hata hivyo mambo haya yanabidi Yatokee mara Kwa mara na yaguse watu nyeti na wakubwa zaidi ili kila tabaka, kila jamaa, kila kundi la hadhi lijue umuhimu wa Katiba mpya.

Sasa najiuliza Spika mpya atakuwa anaamini yeye ni Kiongozi wa Mhimili unaojitegemea kutunga sheria na kuisimamia serikali au ndio atakuwa na hofu ya kilichomkuta mwenzake.

Jambo la hakika ni kuwa, Spika mpya hatakuwa na ujasiri wala kibali cha kujiona katika nafasi ya Kiongozi wa mhimili wa Bunge isipokuwa Hofu ndio itamuongoza.

Nafikiri Kama taifa tunapaswa tuyaangalie mambo haya Kwa maslahi ya nchi.

Wanaosema Hakuna haja ya Katiba mpya wasisubiri yawakute Kama yalivyowakuta wengine.

Hata Ndugai naona sasa anaweza ona Ufa kwenye ukuta uliomuangukia, na hii ni fundisho kwetu sote.

Tunahitaji uzalendo zaidi.
 
Back
Top Bottom