Kwa kinachoendelea TFF kesho wanaweza kukosa mapato

Kwa kinachoendelea TFF kesho wanaweza kukosa mapato

Joined
Oct 26, 2021
Posts
99
Reaction score
294
Unaikumbuka tarehe 25.6.2021 Kilichotokea katika sekta ya michezo Tanzania?! Hahaha acha nicheke kwanza na nishushie maji ya AFYA kidogo uku nikisubiri spare zangu nilizoagizwa pale kariakoo mtaa wa Lumumba kwa bwana GSM nikiendelea kusubiri MO TAMBI anazoandaa shemeji yenu.

Anyways Mechi ya Simba na Yanga imekuwa na mvuto mkubwa sana, si kwa Tanzania tu ata nchi jirani uku ikileta ushawishi mkubwa zaidi na kuwavutia wengi kwa bara la Afrika asa kwa wapenzi wa soka na kabumbu uku wengi wao wakiwaangalia nini watafanya wachezaji wa mataifa yao.

Hii imekwenda mbali na kupelekea kuwa DERBY ya tatu kwa ushawishi na amshaamsha kwa bara la Africa. Na mechi hii inamapato makubwa sana si kwa TFF, selikali na timu husika bali pia kwa watanzania wenyewe ambao ufanya biashara katika eneo la uwanja siku iyo.

Tarehe 25.6.2021 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kulitegemea kufanyika kwa derby nyingine maarufu kwa jina la KARIAKOO DERBY mida ya saa 11 jioni saa za Afrika mashariki. Yanga Afrika walikuwa wa kwanza kufika uwanjani uku wekundu wa Msimbazi wakisema mchezo umesogezwa mbele hadi saa moja pia bado saa moja hakuna timu iliyoingia uwanjani na badae mchezo ule kuharishwa.

Nyenzo zetu bado ziko nyuma; nilichokiwaza zaidi ni kuhusu mda wetu; gharama za viingilio kwa wale wenye mapenzi mema na timu zao waliopata wasaa wa kuingia ndani ya uwanja na kuisubiri mchezo ule ulioarishwa. Hii ilipelekea selikali kuingilia kati; Bunge likasema na kusisitiza zaidi na zaidi. Ila kwa leo sitazungumzia hasara watu, timu pia visununu vilivyokuwepo kwani tofauti zile zilizikwa zamani sana na kumaliza matatizo yale.

Kinachoendelea sasa mpaka mda huu naandika thread hii, kinanipa mashaka makubwa sana kama kweli mchezo wa kesho ni kweli utafanyika kweli au lah?!!! Kwanini?!!! Simba ni taasisi kubwa sana bila shaka Yanga. GSM mdhamini wao mkuu kwa misimu mitatu mfululizo ni GSM uku SIMBA ni Bilionea MO. MO na GSM ni wafanyabiashara ila moja wao kaenda mbali zaidi na kutaka kulikuza zaidi soka la Tanzania na kulifanya kuvutia kwa kuweka mzigo kwenye ligi. Kama mdhamini mwenza anataka nembo yake kuwepo kwenye flana zote za timu ambazo zinacheza ligi anayoidhamini.

Ebu ngoja kwanza tuzungumze na wanasheria kidogo watusaidie katika ili Jambo. Hivi inawezekana kuingia kwenye mkataba na watu ambao utakuwa upo katika pande zote mbili kwa maana ya kwamba upo upande wa offerer na offeree? Wanasheria wanasema any contract should aim at creating good intention when performing it. Sasa bwana GSM hapa nashindwa kuelewa sawa utaperform na TFF ila vipi kuhusu hawa YANGA inamaana unajivisha pande sura mbili at once... anyways tuendelee watatujibu wanasheria.

Leo hii Simba wamegomea press kitu ambacho kimeanza kunipa mashaka kama kweli watakubali kuingiza timu uwanjani. Juzi mkurugenzi mtendaji wa Simba Miss. Barbra aliambatana na wanasheria wakaenda kuhoji uhalali wa logo GSM kuwepo katika fulana zao. Mpaka kufikia pale jezi ya simba imeelemewa na matangazo bado uongeze na ilo mnataka nini lakni GSM?!!!
Watu bado wanawasiwasi na kile kilichotokea 25.6.2021 mchezo kuarishwa na baadhi kukosa kiingilio walichokilipia wakati wa kuingia. Idadi ya mashabiki waliongia katika mechi ile sio sawa na kilichoingia wakati wa marudio wa mechi ile.

TFF wasipoweka sawa suala ili mapema, wenda ikashudia idadi ndogo ya mashabiki kuingia uwanjani kwa kipindi iki uku wengi wao wakohofia yale. Wengi wao wanashauku kuwaona wachezaji wao kwani vikosi viko poa sana kuliko mda wote hasa Yanga ambao walikuwa wakisuasua kwa misimu minne mfululizo. Msimu huu wanapigiwa chapuo kuwa mabingwa wa nchi.
 
Unaikumbuka tarehe 25.6.2021 Kilichotokea katika sekta ya michezo Tanzania?! Hahaha acha nicheke kwanza na nishushie maji ya AFYA kidogo uku nikisubiri spare zangu nilizoagizwa pale kariakoo mtaa wa Lumumba kwa bwana GSM nikiendelea kusubiri MO TAMBI anazoandaa shemeji yenu...
Waliosaini huo mkataba ndio wakulaumiwa wala sio simba.
 
Tff,, inapaswa kuwajibika ktk hili endapo ikijirudia tena kama kipindi kile,, tatizo ni kuwa mpira wa kibongo unaendeshwa kindewa mno,, hata hao viongozi wenyewe wa tff wamewekwa na watu kwa interest zao ili wawatumikie, na ndio mana kwenye chaguzi zao nyingi unaskia mtu kapita bila kupingwa,, so wanatakiwa kulipa fadhila kwa waliowaweka!! Sie yetu macho
 
Tanzania hakuna mpira ni takataka tu.
Bro! Naomba msaada wako maana kuna masuala sijaelewa.

Simba haitaki kuvaa logo ya GSM kwa sababu;-

1. Haifahamu lolote linaloendelea zaidi ya kusikia GSM ni mdhamini mwenza?

2. Haijapokea pesa ya udhamini kutoka hao GSM + TFF?

3. Imepokea pesa lakini haina mkataba baina ya vilabu na TFF + GSM unaoeleza hayo?

4. Inafahamu na imepokea mkataba na pesa lakini ni against kanuni kuvaa mdhamini mwenza?
 
Kikosi kipeleke ombi maalumu shirikisho la soka la Rwanda tuhamie huko , majitu yanafanya mikataba hewa kisa yamepewa cha juu yanajitoa fahamu.

Kwa muda mrefu simba wamekuwa wakichukuliwa kama push over sasa hali hii ikome.

Baada ya kilichoitwa kusaini mkataba wa udhamini, lopolopo lilipost kwamba MPENDE MSIPENDE MTAIVAA NEMBO BEGANI baada ya hapo Tff wakatoa statement ya kupiga marufuku kujadili mkataba huo.

Yaani lopolopo lilikuwa linajua details za maktaba huo wa kishoga ila simba hawajui

Uache bilioni 1 kwa mwaka ya fed vunja bei ukavae takataka za kit supplier wa utopolo kwa milioni 60 kwa mwaka

IMETOSHA KUHUSU HAYA MATAPELI YA TFF NA BODI YA LIGI

TUMEHANGAIKA MIAKA 4 LIGI INASHIKA NAFASI YA 10 AFRIKA NA INAINGIZA TEAMS 4 BAKINI NA MAKOROKOCHO YENU

WALA MSIHANGAIKE KWENDA UWANJANI KESHO HAKUNA MECHI KANUNUENI BIA NA MISHIKAKI HIZO HELA

HONGERENI MATAPELI YA GSM MMEJUA KUVURUGA HALI YA HEWA, MIAKA 3 MMETAPELI HUKO UTOPOLONI SASA MMEONA MKAHONGE MAJITU YENYE NJAA YAHARIBU KILA KITU
 
kikosi kipeleke ombi maalumu shirikisho la soka la Rwanda tuhamie huko , majitu yanafanya mikataba hewa kisa yamepewa cha juu yanajitoa fahamu...
Wakati mkataba unasainiwa viongozi wa simba hawakuwepo????
 
Basi jamani tumekubali nembo ya GSM msivae ila uwanjani mje tucheze mpira. ila mkigoma na hapo tunawafata popote mtakapo kua mmejificha tunavalisha jezi kwa lazima chini ya ulinzi tunawapeleka uwanja wowote uliopo karibu na game inapigwa kwa lazima. Baada ya game hapo mtajijua wenyewe
 
TFF haiwez kuijibu timu moja kwenye vyombo vya habar.......kama hawataki wasije uwanjan kesho....
 
TFF haiwez kuijibu timu moja kwenye vyombo vya habar.......kama hawataki wasije uwanjan kesho....
 
Kikosi kipeleke ombi maalumu shirikisho la soka la Rwanda tuhamie huko , majitu yanafanya mikataba hewa kisa yamepewa cha juu yanajitoa fahamu.

Kwa muda mrefu simba wamekuwa wakichukuliwa kama push over sasa hali hii ikome.

Baada ya kilichoitwa kusaini mkataba wa udhamini, lopolopo lilipost kwamba MPENDE MSIPENDE MTAIVAA NEMBO BEGANI baada ya hapo Tff wakatoa statement ya kupiga marufuku kujadili mkataba huo.

Yaani lopolopo lilikuwa linajua details za maktaba huo wa kishoga ila simba hawajui

Uache bilioni 1 kwa mwaka ya fed vunja bei ukavae takataka za kit supplier wa utopolo kwa milioni 60 kwa mwaka

IMETOSHA KUHUSU HAYA MATAPELI YA TFF NA BODI YA LIGI

TUMEHANGAIKA MIAKA 4 LIGI INASHIKA NAFASI YA 10 AFRIKA NA INAINGIZA TEAMS 4 BAKINI NA MAKOROKOCHO YENU

WALA MSIHANGAIKE KWENDA UWANJANI KESHO HAKUNA MECHI KANUNUENI BIA NA MISHIKAKI HIZO HELA

HONGERENI MATAPELI YA GSM MMEJUA KUVURUGA HALI YA HEWA, MIAKA 3 MMETAPELI HUKO UTOPOLONI SASA MMEONA MKAHONGE MAJITU YENYE NJAA YAHARIBU KILA KITU
Umekaa ukawazaa ukaona uandike huu uharo
 
Back
Top Bottom