Vya cherehani vingapi?
Vya kushona na mkono vingapi?
Uchumi wa viwanda oye.
Mkoa wa Pwani pekeyake unajumla ya viwanda 260 vipya
MUHTASARI WA ORODHA YA VIWANDA MKOA WA PWANI NI KAMA IFUATAVYO:-
(a) Jumla ya Viwanda Vikubwa, vya Kati na Vidogo 260 vimejengwa kama ifuatavyo (Mkuranga viwanda 54, Kibaha Vijijini viwanda 76, Kibaha Mji viwanda 71, Chalinze viwanda 32, Bagamoyo viwanda 18, Kisarawe viwanda 4 na Mafia viwanda 5. Viwanda vingi Chalinze ni vya kokoto(Quarry) na Kibaha ni vya Matofali.
Angalia Kiambatisho A.
Vifuatavyo ni baadhi yaviwanda vikubwa vilivyopo Mkoa wa Pwani:-
(i) Kiwanda cha Vigae (Tiles) cha Goodwill (Tanzania) Ceramic Co., Ltd kilichopoMkuranga. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Mwekezaji kutoka nchini China, na kinatarajiwa kuanza uzalishaji wa Mapema 2017
(ii) Kiwanda cha Nondo cha Mohamed Kiluwa Group and Company Ltd cha Mlandizi ambacho kinatarajiwa kuanzauzalishaji mapema 2017.
(iii) Kiwanda cha Kusindika matunda, (Sayona Fruits)kilichopo Kijiji cha Mboga - Chalinze - Bagamoyo. Mwekezaji ni Makampuni ya MMI (Motisun Group) ambayo yatawekeza jumla ya Dola za Kimarekani milioni 55. Kiwanda kinaendeleakujengwa na kitakamilika Oktoba, 2017.
(iv) Kiwanda cha Sarujiitakayojulikana kama “Mamba Cement” kilichopo Kijiji cha Talawanda na Magulumatali- Bagamoyo. Mwekezaji niMakampuni ya MMI (Motisun Group). Nao pia kibali cha ujenzi kimepatikana na ujenzi uko mbioni kuanza.
(v)Kiwanda cha Nondo cha MMI Intergrated Steel Mill kilichopo eneo la Zegereni, Halmashauri ya Mji Kibaha. Mwekezaji amepewa kibali cha ujenzi na ujenzi utaanzawakati wowote.
(vi) Kiwanda cha Kuunganisha Magari ya Zimamoto na Matrektacha ubia kati ya SUMA JKT na EQUATOR Automech Co. Ltd. na kuunda Kampuni iitwayo
“EQUATOR SUMAJKT LIMITED”.
· Wataunganisha magari ya zimamoto kwa kushirikiana naKampuni ya ST AUTO iliyopo nchini Russia.
· Magari yatatengenezwa kwa kutumia viwango vya Kimataifa.
· EQUATOR SUMAJKT LTD itakuwa ni kiwanda cha pili katika Bara la Afrika, cha kwanzakipo Afrika ya Kusini.
· Ajira zitakazotengenezwa ni 200
· Eneo la kiwanda ni Ekari 63, zipo Ruvu JKJ
· Kiwanda kimekamilika, kitaanza ‘Operation” Januari, 2017.
(vii) Kiwanda cha Elven Agria Company Ltd. kinajengwa Mapinga Bagamoyo kwa ajili yaukaushaji wa matunda ya aina mbalimbali. Kiwanda kitafunguliwa Januari, 2017.
(viii) Kiwanda cha Kusindika Matunda cha Kampuni ya Bakhresa Food Products Ltd.kimezinduliwa Septemba, 2016.
(ix) Kiwanda cha Vigae (Tiles) cha Kampuni ya TWYFORD (Tanzania Ceramic Tiles Factory) kutoka China kinachojengwa eneo la Pingo katika Halmashauri ya Chalinze, Bagamoyo.Kitatengeneza ajira za moja kwa moja (direct) 2,000 naajira nyingine 4,000 ambazo siyo za moja kwa moja (indirect). Ujenzi wa Kiwanda unaendelea na kinatarajia kuanza uzalishaji tarehe 1Julai, 2017 .
(x) Kiwanda cha Sabuni ya Unga cha Kampuni ya KEDS (T) CO LTD kutoka China kinachojengwaeneo la Viwanda la Mkoani katika Halmashauri ya Mji Kibaha. Ujenzi wa Kiwandaunaendelea na kinatarajia kuanza uzalishaji Mwezi Juni, 2019
(xi) Kiwanda cha kuunganisha matrekta TAMCO katikaHalmashauri ya Mji Kibaha. Kimeanza ujenzi Mwaka 2017 Kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2017.mradi huu utagharimu kiasi za dola za kimarekeni milioni 55 pindi utakapokamilika,ukijumuisha ujenzi wa kiwanda cha matrekta na mitambo yake, vituo nane kwaajili ya huduma kwa wateja( service centers) mafunzo kwa wafanyakazi na manunuzi kwa vifaa vya kuunganishia matrkta jumla ya 2,400
(xii) GLOBAL PACKAGING (T) LTD: Kiwanda hiki kilianza kujengwa mwaka 2015 na kuanza uzalishaji mwaka 2016. Kiasi cha Billion 7.6 zimewekezwa, Kiwanda kipo Halmashauri ya Mji Kibaha. Mmiliki wa kiwanda hiki ni Wande Printing andPackaging Co. LTD na NDC.
(xiii) Kiwanda cha kuunganishaBodi za Magari cha BENBROS kipo katika hatua ya kutwaa ardhi katika Halmshauri ya Wilaya ya Kibaha.
Chanzo; pwani.go.tz/project-details/viwanda