Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pesa chafu ni ile iliyopatikana kwa njia haramu (ujambazi, wizi, rushwa, uharamia etc). Usafishaji wa pesa chafu, ni shughuli halali ambayo mtu anaifanya kwa kutumia (mtaji wa) pesa chafu, ili baadae pesa inayotakana na shughuli hiyo ionekane imepatikana kihalali (safi). Kwa mfano mtu umekwiba mipesa serikalini huko, anaingiza pesa hiyo kama mtaji kwenye biashara halali na kisha kuanza kutumia pesa/faida inayotokana na biashara hiyo. Kwa wasiojua kuwa mtaji ulitokana na pesa chafu, wataona huyo 'mwizi' anatumia pesa halali aliyoipata kutokana na biashara yake. Zipo njia nyingi za kusafisha pesa, huo mfano niliotoa ni mojawapo tu ya njia hizo.Heshima mbele wakuu wangu!
Naomba msaada kwenye hili.....hivi mtu anaposhtakiwa kwa kosa la kutakatisha pesa chafu.....maana yake nini? Pesa chafu ndio zilizopatikanaje? Shukran.....nasubiri majibu yenu.:baby:
Pesa chafu ni ile iliyopatikana kwa njia haramu (ujambazi, wizi, rushwa, uharamia etc). Usafishaji wa pesa chafu, ni shughuli halali ambayo mtu anaifanya kwa kutumia (mtaji wa) pesa chafu, ili baadae pesa inayotakana na shughuli hiyo ionekane imepatikana kihalali (safi). Kwa mfano mtu umekwiba mipesa serikalini huko, anaingiza pesa hiyo kama mtaji kwenye biashara halali na kisha kuanza kutumia pesa/faida inayotokana na biashara hiyo. Kwa wasiojua kuwa mtaji ulitokana na pesa chafu, wataona huyo 'mwizi' anatumia pesa halali aliyoipata kutokana na biashara yake. Zipo njia nyingi za kusafisha pesa, huo mfano niliotoa ni mojawapo tu ya njia hizo.