SoC04 Kwa kutizamia mafanikio, changamoto za sekta mbalimbali; Haya yafanyike kwa maendeleo ya taifa

SoC04 Kwa kutizamia mafanikio, changamoto za sekta mbalimbali; Haya yafanyike kwa maendeleo ya taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

mwalimuproto

Member
Joined
Apr 23, 2024
Posts
12
Reaction score
1
TANZANIA TUITAKAYO
Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika inayoendelea kukua kwa kasi kiuchumi. Hii ni kutokana na umahiri wa awamu mbalimbali za uwongozi wa serikali zenye ustadi na umahiri mkubwa wa kusimamia na kuratibu shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Zifuatazo ni tathmini juu ya sekta mbalimbali nchini.
1. ELIMU
Mafanikio

● ujenzi wa madarasa kwa shule zote nchini kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia mashuleni.
● kuboreshwa kwa mfumo wa utoaji na upokeaji wa mikopo kwa ngazi ya stashahada na shahada.
● kutolewa kwa fursa za kielimu zenye lengo la kukuza elimu nchini. Mfano, kupitia fursa ya "SAMIA SCHOLARSHIP ".
● Maboresho ya taasusi mbalimbali kwa elimu ya kidato cha sita
● utolewaji wa elimu bila malipo.
Screenshot_20240501_172657_Google.png

-Kielelezo kuonyesha picha ya madarasa mapya
Changamoto
● kiwango kidogo cha pesa inayotolewa kama mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Hivyo kupelekea idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa gharama za kujiendesha kielimu na kufanya maamuzi ya kusitisha masomo.
● upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hesabati, hivyo kuelekea wanafunzi wengi kutokufanya vizuri kwenye masomo ya sayansi na hisabati.
● upungufu wa nyumba za waalimu
● uhaba wa miundombinu rafiki ya kujifunzia mashuleni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
● matumizi ya dhana za kifundishia zisizo endana na kasi ya ukuaji wa teknolojia.
Nini kifanyike
kuongezwa kwa pesa ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
● kuboreshwa kwa miundombinu ya kujifunzia mashuleni. Mfano, ukarabati wa madarasa.
● kuongezwa kwa idadi ya waalimu wa masomo ya sayansi na hesabati mashuleni
2. KILIMO NA UFUGAJI
Mafanikio

● uvumbuzi wa aina mbalimbali za mbegu kwa lengo la kukuza uzalishaji wa mazao bora
kutolewa kwa mikopo nafuu kwa wakulima wadogo wadogo.
● kujengwa kwa machinjio ya kisasa . Mfano, machinjio ya vingunguti,Dar es salaam .
● kuhimarisha huduma za ugani. Mfano, maafisa ugani kupewa pikipiki za kusafiria.
● utoaji na ugawaji wa mbolea za ruzuku kwa bei nafuu kwa wakulima.
● kutolewa kwa elimu juu ya matumizi bora ya ardhi kwa lengo la kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji.
Screenshot_20240501_173926_Google.png

(a) kielezo kuonyesha mifugo
Screenshot_20240501_173802_Google.png

(b) kielelezo kuonyesha mazao bora ya mahindi
Changamoto
upungufu wa wataalamu wa kilimo na ufugaji.
● matumizi ya dhana duni za kilimo na ufugaji zisizoendana na kasi ya kukua kwa sayansi na teknolojia.
Nini kifanyike
kuboreshwa kwa mifumo ya kilimo na ufugaji kulingana na kukua kwa sayansi na teknolojia nchini.
● kupanuliwa kwa masoko nchini kwa lengo la wakulima na wafugaji kuwa na masoko ya uhakika kwa uuzaji na usambazaji wa mazao yao.
● kuongezwa jitihada ya utolewaji wa elimu ya kilimo na ufugaji kwa wakulima na wafugaji wadogo wadogo.
3. MAZINGIRA
Mafanikio

● kuwepo kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi. Mfano, kutengwa kwa maeneo kwaajili ya uhifadhi wa mazingira kama vile Ngorongoro.
● kuendeshwa kwa kampeni ya kuachana na matumizi ya nishati hatarishi kwa mazingira kama vile mkaa na kuni.
Screenshot_20240501_175432_Google.png

-kielelezo kuonyesha nishati mbadala
● kuanzishwa kwa kampeni mbalimbali za kushirikisha jamii katika utunzaji wa mazingira.
Screenshot_20240501_174615_Google.png

- kielelezo kuonyesha ushiriki wa jamii kwenye kutunza mazingira
Changamoto
● Gharama kubwa ya nishati mbadala, hivyo kupelekea kuendelea kutumika kwa nishati hatarishi kwa mazingira.
● kukithiri kwa shughuli mbalimbali za kijamii zinazo pelekea uharibifu mkubwa wa mazingira. Mfano, uchimbaji holela wa madini na uvuvi haramu.
Nini kifanyike
● kuboreshwa kwa mifumo ya utoaji wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira.
● kupunguzwa kwa gharama ya nishati mbadala kama vile gesi asilia.
4. AFYA
Mafanikio
kuongezwa kwa bajeti ya ununuzi wa vifaa tiba na madawa kwa bohari ya taifa ya madawa na vifaa tiba" MSD".
Screenshot_20240501_175104_Google.png

- kielelezo kuonyesha bohari ya dawa na vifaa tiba.
● Utolewaji wa huduma ya afya kwa wazee na watoto bure.
● kuboreshwa kwa miundombinu ya afya vijijini kwa kujengwa zahanati mbalimbali.
Screenshot_20240501_173341_Google.png

-kielelezo kuonyesha ujenzi wa zahanati
Changamoto
Upungufu wa madawa na vifaa tiba kwenye vituo vingi vya afya nchini.
● Upungufu wa wataalamu wa afya mahospitalini.
● huduma zinazotolewa kutokuendana na kasi ya kukua kwa teknolojia.
Nini kifanyike
kuongezwa kwa wataalamu wa afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
● Maboresho ya bima za afya kulingana na kasi ya maendeleo.
● kuboreshwa kwa mifumo ya utoaji huduma kulingana na kasi ya kukua kwa teknolojia.
5. MIUNDOMBINU NA USAFIRISHAJI
Mafanikio
kuboreshwa kwa huduma za usafirishaji wa watu na mali zao kupitia mamlaka ya usafirishaji SUMATRA.
● kujengwa kwa makutano ya barabara za juu " KIJAZI INTER-CHANGR" na mradi wa mabasi yaendayo kasi( Mwendokasi) kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari, Dar-es-salaam.
Screenshot_20240501_172343_Google.png

- kielelezo kuonyesha makutano ya barabara za juu
● kujengwa njia ya reli ya kutumia umeme "SGR" kwa lengo la kuboresha usafirishaji nchini .
Screenshot_20240501_172439_Google.png

- kielelezo kuonyesha reli ya umeme
● Kujengwa kwa mradi mkubwa wa kufulia umeme wa mwalimu nyerere( Julius Nyerere Hydropower Project).
Screenshot_20240501_172528_Google.png

Changamoto
kuchelewa kumalizika kwa miradi mbalimbali kwa wakati kwa mfano, mradi wa " JNHPP".
● Kujengwa kwa miundombinu chini ya viwango hivyo kupelekea kudumu kwa muda mfupi na kuharibika kirahisi.
Nini kifanyike
Kuzingatiwa ubora wa miundombinu kabla ya makabiziano baina ya serikali na wakandarasi.
● Jamii kushiriki ipasavyo kwenye kulinda na kutunza miundombinu nchini.
Kwa kumalizia, serikali kwa kushirikiana na jamii. Zielendelee kutengeneza mikakati wezeshi kwa lengo la kuboresha na kukuza maendeleo ya taifa letu.
MAZINGATIO
picha zilizo tumika kama vielelezo, chanzo chake ni kupitia mitandao ya kijamii. Yaani "Google ".
 
Upvote 4
Kujengwa kwa mradi mkubwa wa kufulia umeme wa mwalimu nyerere
Hili likikamilika kikamilifu = maisha bora kwa kila mtanzania

kuongezwa kwa bajeti ya ununuzi wa vifaa tiba na madawa kwa bohari ya taifa ya madawa na vifaa tiba" MSD".
Iendane na kuboresha matumizi ya TEHAMA kuoata takwimu sahihi kuzuia ukosafu na uharibifu wa dawa.
Gharama kubwa ya nishati mbadala, hivyo kupelekea kuendelea kutumika kwa nishati hatarishi kwa mazingira.
Kweli kaka, tafiti zinahitajika hapa. Nishati mbadala inapaswa kuwa ya nafuu zaidi.

Na kama sio nafuu zaidi basi wananchi tutabakia na hizohizo tunazoziweza hii wala sio sayansi ya maroketi.
 
Mkuu, kuna tatizo la kushindwa kuvote kwenye andiko langu ss nimejaribu kuwasiliana na jamiiforum but bado changamoto inaendelea.
 
Back
Top Bottom