Kwa kuwa hawana ajenda CHADEMA yaamua kucheza na akili za watu kwa gia ya Katiba Mpya

inspectorbenja

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
597
Reaction score
651
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa hali ya siasa ilivyo kwa sasa CHADEMA wameshindwa kupata ajenda ya kuwafanya watanzania washawishike kuwa wao ni mbadala na hii ni kutokana na ukweli kwamba watanzania saa hizi wamepitia tawala za aina zote.

Zama za Kikwete (Mwanadiplomasia aliyetukuka Mungu ampe maisha marefu) CHADEMA walikosoa sana Serikali na kusema ni legelege,imejaa wapigaji,Rais anachekachkea.

Bahati mbaya au nzuri tukapata Rais ambaye alikuwa anaogelea kwenye wimbo uliopigwa na CHADEMA miaka nenda miaka rudi. Cha moto tulichokiona kila mtu ni shahidi.

Kwa sasa watanzania hakuna unachoweza kuwadanganya. Wameona kila kitu- they have seen it all.

Kwa kujua hilo CHADEMA wamekuja na ajenda ya katiba mpya maana hawana sera yoyote mpya.

Ni wakati wa kuwapuuza CHADEMA mazima.
 
Huko kwenu bei ya mafuta yana soma bei gani? tuanzie hapo kwanza.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa hali ya siasa ilivyo kwa sasa.Chadema wameshindwa kupata ajenda ya kuwafanya watanzania washawishike kuwa wao ni mbadala.Na hii ni kutokana na ukweli kwamba watanzania saa hizi wamepitia tawala za aina zote.Zama za kikwete (Mwanadiplomasia aliyetukuka Mungu ampe maisha marefu) chadema walikosoa sana serikali na kusema ni legelege,imejaa wapigaji,rais anachekachkea.Bahati mbaya au nzuri tukapata rais ambaye alikuwa anaogelea kwenye wimbo uliopigwa na chadema miaka nenda miaka rudi.Chamoto tulichokiona kila mtu ni shahidi.
Kwa sasa watanzania hakuna unachoweza kuwadanganya.Wameona kila kitu- they have seen it all.
Kwa kujua hilo chadema wamekuja na ajenda ya katiba mpya maana hawana sera yoyote mpya.
Ni wakati wa kuwapuuza chadema mazima.
Tatizo la Tanzania tuna watu wasioona mbali. Huwezi kuwa na ajenda yenye kuleta maendeleo kama mifumo ya kisiasa katika nchi imekaa kulinda tabaka fulani la watu badala ya kutetea wananchi wote. Inachofanya chadema ni kuondoa ujinga uliozoeleka kwamba mtawala ndie alpha na omega. Lazima nchi iongozwe kwa utaratibu unaoeleweka na sio mtu anajiamulia atakacho. Hivyo uelewe dai la katiba sio Jambo dogo na sio kitu cha kuhusisha na mawazo mepesi mepesi ya kibinafsi. Katiba ndio msingi wa uendeshaji nchi. Mtu mmoja hapaswi kulimbikiziwa mamlaka ya kimaamuzi , lazima kuwepo na kidhibiti mwendo. Mateso, maumivu, na uovu tuliouona siku zilizopita yalikuwa madhara ya katiba yenye mapunguvu. Watu wengi wameporwa haki zao kwa sababu hizo, tumekuwa na viteule vilivyojihusisha na ujambazi kwa vile katiba haikuwa na namna ya kuthibiti teuzi kama hizo. TAMBUA KATIBA NI KWA AJILI YA WATANZANIA. NA SASA NDIO WAKATI WAKE. TUNAHITAJI KATIBA MPYA SASA.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa hali ya siasa ilivyo kwa sasa.Chadema wameshindwa kupata ajenda ya kuwafanya watanzania washawishike kuwa wao ni mbadala.Na hii ni kutokana na ukweli kwamba watanzania saa hizi wamepitia tawala za aina zote.Zama za kikwete (Mwanadiplomasia aliyetukuka Mungu ampe maisha marefu) chadema walikosoa sana serikali na kusema ni legelege,imejaa wapigaji,rais anachekachkea.Bahati mbaya au nzuri tukapata rais ambaye alikuwa anaogelea kwenye wimbo uliopigwa na chadema miaka nenda miaka rudi.Chamoto tulichokiona kila mtu ni shahidi.
Kwa sasa watanzania hakuna unachoweza kuwadanganya.Wameona kila kitu- they have seen it all.
Kwa kujua hilo chadema wamekuja na ajenda ya katiba mpya maana hawana sera yoyote mpya.
Ni wakati wa kuwapuuza chadema mazima.
 
Kuna wakati CCM wajitahidi kutafuta watu wenye weredi Kwenye propaganda kuliko kama mleta mada.
 
Mkuu nakushangaa sana kwa kuona jambo la katiba mpya ni dogo kwako.Jaribu kuangalia na kesho, siyo leo tu.Najua kwa sasa unaonekana kuwa mnufaika wa katiba iliyopo lakini kesho yako huijui hivyo katiba hii unayo ona inafaa inaweza kukutia ktk kilio kikuu hadi uka shangaa.Ndiyo maana watu wanaoona mbali wanataka nchi iwe na katiba itakayo wafanya wajue kwa uhakika kesho yao itakuwaje.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa hali ya siasa ilivyo kwa sasa.Chadema wameshindwa kupata ajenda ya kuwafanya watanzania washawishike kuwa wao ni mbadala.Na hii ni kutokana na ukweli kwamba watanzania saa hizi wamepitia tawala za aina zote.Zama za kikwete (Mwanadiplomasia aliyetukuka Mungu ampe maisha marefu) chadema walikosoa sana serikali na kusema ni legelege,imejaa wapigaji,rais anachekachkea.Bahati mbaya au nzuri tukapata rais ambaye alikuwa anaogelea kwenye wimbo uliopigwa na chadema miaka nenda miaka rudi.Chamoto tulichokiona kila mtu ni shahidi.
Kwa sasa watanzania hakuna unachoweza kuwadanganya.Wameona kila kitu- they have seen it all.
Kwa kujua hilo chadema wamekuja na ajenda ya katiba mpya maana hawana sera yoyote mpya.
Ni wakati wa kuwapuuza chadema mazima.
Ni punguani pekee anayeweza kuwa mfukoni mwa mwenyekiti wa hilo genge la Ufipa. Hilo genge la wahuni sasa limeanza kuamka,watakuja kwa njia moja ila watatawanyika kwa njia saba.
 
Back
Top Bottom