Kwa lengo la kusaidia jamii

Kwa lengo la kusaidia jamii

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2008
Posts
777
Reaction score
50
Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini unafanya hicho unachokifanya?Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini ulijiunga na jamii forums? Ulishawahi kujiliuza ni kwa nini uliamua kusomea fani uliyosomea? Na je ulishawahi kufanya kitu kwa lengo la kuisaidia jamii?

Wengi wetu hatujui ni kwa kiasi unakuwa karibu na mafanikio pale unapofanya jambo lako huku ukiwa na lengo la kuisaidia jamii inayokuzunguka au uliyotoka?Yaani kabla ya kufanya jambo lako ukaifikiria kwanza jamii inayo kuzunguka na kujaribu kudadafua ni kwa kiasi gani jamii hiyo itanufaika na jambo lako hilo na si wewe utanufaika vipi! Kwa mfano ukitaka kuanzisha biashara,ukataka kwenda kuongeza elimu au kuanzisha gazeti,ukafikiria kwanza jamii itanufaika vipi na biashara yako,kusoma kwako au gazeti lako.

Wakati mwingine unaweza kugundua jamii inayokuzunguka ina tatizo ambalo wewe unaweza kusaidia bila ya kupata hasara yoyote.Mfano,jamii inayokuzunguka ina tatizo kubwa la maji na wewe una uwezo wa kuweka bomba la maji mbele ya nyumba yako na kuwauzia maji hayo kwa bei nafuu, au tatizo la gharama za kunyoa nywele zilivyo juu kwa sasa,na unajua kabisa kwamba wanajamii wengi hawawezi kunyoa kwa 1500/= kwa kichwa ili hali una uwezo wa kuanzisha salon itakayowatoza wananchi 700/= kwa kichwa au 500/= na bado saloon ikaweza kujiendesha,kumbuka hapa lengo lako si faida bali ni kutatua tatizo.

Swali langu hapa ni je ulishawahi kuifikiria jamii inayokuzunguka au jamii unayotoka?ukawasaidia hata kwa namana ya mifano hapo juu.Si vibaya tukaanza kufikiria katika yale tulokwisha yafanya jamii imenufaika vipi na katika yale tunayotarajia kuyafanya jamii itanufaika vipi.Ni ukosefu wa fikra hii plus ubinafsi ndo maana ufisadi unatamalaki hasa katika nchi zetu hizi za kibepari
 
Back
Top Bottom