SoC04 Kwa leo na kesho yetu bora, elimu ya sarafu pepe itolewe

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mchina5

New Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
2
Reaction score
2
Dunia iko katika mapinduzi ya nne ya viwanda ambapo msingi wake mkubwa ni Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHEMA), Maendeleo ya Teknolojia na Mawasiliano yameleta mambo mengi sana duniani hasa kuibuka kwa sarafu za kidigitali (Cryptocurrency and Blockchain technology), Hivyo kama nchi hatuna budi kwenda sambamba na uelekeo wa dunia ili tusiachwe nyuma na kupitwa na fursa zinazotokana na sarafu mtandao na Blockchain.

Wakati tunaelekea katika dira mpya ya maendeleo ya miaka 25 ijayo (2025-2050) ni vyema suala la sarafu mtandao likajumuishwa na elimu ikatolewa kwa wananchi ili tusiwe kisiwa kilichotengwa na dunia.

Sarafu mtandao au sarafu pepe ni nini?
Ni pesa au sarafu ya kidijitali iliyo mtandaoni, hivyo ni sawa na kuiita sarafu pepe.Mfano wa sarafu ya mtandao ni kama barua ya mtandao inayoitwa barua pepe.

Sarafu pepe inafanya kazi bila kutegemea mamlaka kuu, mfano pesa zako kwa kawaida zinasimamiwa na serikali kupitia mabenki ambayo yanaamua thamani yake kupanda au kushuka kwa kutumia vigezo mbalimbali, sarafu pepe haina msimamizi, imegatuliwa (Decentralized) yaani haidhibitiwi na chombo chochote na badala yake shughuli zinarekodiwa kwenye kumbukumbu au leja ya kidijitali inayoitwa Blockchain na Node ni mtandao wa kompyuta unaotunza Blockchain.

Sarafu pepe zilianza lini?
Wazo la matumizi ya sarafu pepe lilianza mwaka 2008 baada ya mtikisiko wa kiuchumi ulioikumba dunia kwa wakati huo ila utekelezaji wake ulianza mwaka 2009 kwa kuzinduliwa kwa Bitcoin ikiwa ndio sarafu ya kwanza kutokea katika uso wa dunia ingawa mmiliki wa Bitcoin hajulikani ni nani na anatokea wapi na hajulikani aidha ni mtu mmoja au kikundi cha watu ila amepewa jina la Satoshi Nakamoto.

• Mnamo mwaka 2009, wakati Bitcoin inatolewa kwa mara ya kwanza, sarafu 50 ziliweza kupatikana bure kwa kuchimbwa (online mining)kwa dakika 10,Hadi kufikia Mei 2024 sarafu moja ya Bitcoin ilifikia thamani ya dola za kimarekani 67000/=

• Litecoin coin ilipozinduliwa mwaka 2011, Litecoin 100 ziliweza kupatikana bure kila siku, Hadi kufikia Mei 2024 LTC moja ilikuwa thamani ya zaidi ya dola 450 za Kimarekani.

• Ethereum ilipozinduliwa Kwa mara ya kwanza mwaka 2014, 30ETH zilichomwa bila malipo na hadi kufikia Mei mwaka 2024 sarafu moja ya Ethereum iliuzwa kwa zaidi ya dola za kimarekani 4868.
Hizo ni chache kwa kuzitaja.

Faida za sarafu pepe kwa wananchi na serikali ni zipi?

Faida ya kwanza ni kwa kufanya biashara ya kununua na kuuza sarafu, Sarafu pepe zinakawaida ya kupanda na kushuka (votality)Mtu au taasisi za serikali zinaweza kununua aina fulani ya sarafu ingali bei ya chini na kuuza pale bei unapopanda, Mfano Bitcoin sasa ina thamani ya dola za kimarekani zaidi ya 60,000/ lakini miaka miwili nyuma ilikuwa chini ya dola 30,000/.

Faida ya pili ni kwa kuagiza bidhaa nje ya nchi kwa malipo ya sarafu pepe. Hii ni njia rahisi ya kukabiliana na upungufu wa fedha za kigeni kama ambavyo nchi katika nyakati tofauti tofauti imekuwa ikikumbwa na kadhia hiyo,Mfano Ufalme wa Saudi Arabia imekataa kusaini mkataba mpya na serikali ya Marekani mkataba wa Petro dollar uliodumu kwa miaka 50 kutoka Juni 8. 1974 hadi Juni 8. 2024 ambapo mauzo ya mafuta ilikuwa ni kwa malipo ya dola za Marekani,sasa Saudi Arabia inaangalia kupokea malipo kwa fedha zingine kama EURO, POUND,YUAN na sarafu za kidijitali ikiwemo Bitcoin ili kupanua wigo wa kibiashara.

Your browser is not able to display this video.


Faida tatu ya sarafu pepe inawezesha ufikiwaji wa huduma za kifedha hata katika mazingira ambayo miundombinu yake ni mibovu au iwe hata hakuna kabisa huduma za kibenki.

Faida ya nne ya sarafu pepe ni biashara ya faragha,Mfano mtu anaweza kununua au kuuza bidhaa bila kujulikana mnunuzi ni nani au gharama za fedha zilizotumika.

Faida ya tano ya sarafu pepe ni kwa kuwekeza na kuzishikilia kuiwango fulani cha sarafu katika wallet(E-wallet) yaani,(Staking)ili zitumike katika uendeshaji wa miradi wa kidijitali na kupata gawio kupitia faida.

Faida sita ni kupitia kutengeneza, kununua na kuuza rasilimali za pekee(NFTs) kama vile kazi za sanaa kama muziki,filamu katika majukwaa ya Cheni mnyororo (Blockchain),Wasanii wanaweza kunufaika na kazi za sanaa kwa kupata malipo makubwa bila kuzingatia mipaka ya nchi.

Sarafu pepe zina changamoto zipi?
Ni vyema pia na changamoto zikafahamika ili wananchi wajue namna bora ya kuziendea sarafu za kidijitali kama hata Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alipozungumzia sarafu pepe katika maadhimisho ya siku ya uhuru 9.12.2023.

"Maendeleo ya Teknolojia duniani yanaambatana na fursa na changamoto, Mfano, masuala ya akili bandia, teknolojia ya sarafu za kidijitali na hitajio la nishati mbadala,inaweza kuwa fursa au changamoto kwetu,tukiwa na uelewa wa mambo na mipango mizuri,tunaweza kutumia fursa hizo kwa maendeleo ya nchi yetu,na tusipokuwa na mipango mizuri inaweza kuwa changamoto kwa taifa letu" sehemu hotuba yake kwa ufupi.

Changamoto za sarafu pepe ni kama zifuatazo;

• Hakuna uthibiti wa thamani yake. Mfano, unaweza kulala Bitcoin ikiwa na thamani ya dola za kimarekani 20,000/ na kuamka asubuhi na ukakuta thamani imeshuka na kufikia dola 4000 au chini zaidi, hivyo ni vyema kujua ni muda upi sahihi wa kununua na kuuza ili kuepuka hasara.

• Sarafu pepe zimehusishwa na biashara nyingi haramu mitandaoni, kwakuwa mifumo yake ya biashara ina usiri mkubwa hivyo watu waovu linaweza kuwa jukwaa lao la kufanya uovu hivyo ni vyema serikali yetu ikaweka mifumo kizuri mapema ili kukabiliana na changamoto hii pindi sarafu pepe itakaposhika kasi.
• Mmiliki yeyote yule wa sarafu pepe anapewa ufunguo kwa njia ya code unaotumia kuingia kwenye akaunti yako, hivyo ukipoteza code hizo hakuna namna yoyote ya kuikomboa akaunti yako na hapo unapoteza sarafu zako milele.
,
Hitimisho, ni vyema elimu ya sarafu pepe ikatolewa, serikali ina jukumu hili ikishirikiana na taasisi zisizo za kiserikali pamoja na mtu mmoja mmoja wenye ujuzi wa masuala ya sarafu pepe na Blockchain kama ambavyo Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alipoisisitiza B.O.T kupitia Gavana wake wakati wa uzinduzi wa jengo la B.O.T jijini Mwanza kujiandaa na wimbi la sarafu pepe ili kuwa tayari na mabadiliko makubwa ya teknolojia ya fedha.
Aidha nawaasa wananchi kuchangamkia fursa mapema za sarafu pepe hasa sarafu za mtandao wa Pi ambazo kwa sasa zinapatikana bure kabla ya uzinduzi wake mwishoni mwa mwaka huu 2024.

Imeandaliwa na Athumani Juma Athumani
0764711825/0683407711
jathumani659@gmail.com
 

Attachments

  • inbound2901831182580279676.mp4
    9.6 MB
  • inbound7905448810444543663.mp4
    2.3 MB
Upvote 6
watu watakuja tena kuchangia huu uzi kwa fujo siku mtu mwenye Pi coins kadhaa ajenge nyumba----------------muda utaongea,Inshallah
 
watu watakuja tena kuchangia huu uzi kwa fujo siku mtu mwenye Pi coins kadhaa ajenge nyumba----------------muda utaongea,Inshallah
Mkuu kuna group letu la Pi nipe namba yako ya whatsapp nkuadd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…