Kwa maandalizi hafifu ya kuandaa AFCON, Rwanda atachukua nafasi yetu Tanzania

Kwa maandalizi hafifu ya kuandaa AFCON, Rwanda atachukua nafasi yetu Tanzania

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Tujikumbushe nchi zilizoshinda bid ya kuandaa mashindano ya AFCON 2027 ni TANZANIA, KENYA NA UGANDA lakini sisi hapa nyumbani tunaongea sana kuliko vitendo.

Nchi nyingine KENYA NA UGANDA wako site wanajenga na kukarabati lakini sisi tuko busy kuunda kamati za AFCON na kulipana posho tu lakini hakuna kinachoendelea.

Jirani yetu RWANDA hakupata fursa ya kuandaa mashindano lakini Yuko busy anajenga viwanja na kukarabati vya zamani.

Naamini RWANDA ana uhakika TANZANIA tutakalia maneno na mambo ya kamati lakini hatutafanya lolote.

RWANDA ni mjanja anajua ukubwa na umuhimu wa mashindano haya kucheza nchini kwake na laZima atawashawishi CAF kuhamishia mashindano RWANDA badala ya TANZANIA

Natabiri AFCON itafanyika RWANDA, KENYA NA UGANDA

Screenshot_20240705-194721.png
 
Daah! Nchi inazidi kuwa ngumu kila kukicha makodi lukuki, umeme sasa kulipia mwezi 2000 🤔
 
Picha zote ulizojaza za rwanda. Ni za uwanja mmoja tu amahoro stadium.

Rwanda wana uwanja wa maana mmoja tu ambao ndio huo wana ukarabati.

Sijui kwa nini wabongo mnaikuza sana rwanda.

Hiyo nchi tumewaacha mbali kwenye kila kitu.

Yaani tuache kufanya finishing ya bwawa la umeme kubwa kuliko yote africa mashariki na la nne kwa ukubwa barani africa. Lenye thamani ya trilioni 7 tuanze kufikiria upuuzi wa rwanda. Tanzania Tupo busy now na kuwasha mtambo namba 7 wa bwawa la umeme letu.

Tupo busy na kuwasha treni ya umeme ya pekee kwenye nchi zote africa mashariki. Trilioni 16 zimewekwa pale.
Ambayo Rwanda itamchukua miaka 100 kuja kuipata treni ya umeme
 
Tujikumbushe nchi zilizoshinda bid ya kuandaa mashindano ya AFCON 2027 ni TANZANIA, KENYA NA UGANDA lakini sisi hapa nyumbani tunaongea sana kuliko vitendo.

Nchi nyingine KENYA NA UGANDA wako site wanajenga na kukarabati lakini sisi tuko busy kuunda kamati za AFCON na kulipana posho tu lakini hakuna kinachoendelea.

Jirani yetu RWANDA hakupata fursa ya kuandaa mashindano lakini Yuko busy anajenga viwanja na kukarabati vya zamani.

Naamini RWANDA ana uhakika TANZANIA tutakalia maneno na mambo ya kamati lakini hatutafanya lolote.

RWANDA ni mjanja anajua ukubwa na umuhimu wa mashindano haya kucheza nchini kwake na laZima atawashawishi CAF kuhamishia mashindano RWANDA badala ya TANZANIA

Natabiri AFCON itafanyika RWANDA, KENYA NA UGANDA

View attachment 3034470
Kuandaa AFCON unahitaji kuwa na viwanja vingapi kwani
 
Picha zote ulizojaza za rwanda. Ni za uwanja mmoja tu amahoro stadium.

Rwanda wana uwanja wa maana mmoja tu ambao ndio huo wana ukarabati.

Sijui kwa nini wabongo mnaikuza sana rwanda.

Hiyo nchi tumewaacha mbali kwenye kila kitu.

Yaani tuache kufanya finishing ya bwawa la umeme kubwa kuliko yote africa mashariki na la nne kwa ukubwa barani africa. Lenye thamani ya tririoni 7 tuanze kufikiria upuuzi wa rwanda. Tanzania Tupo busy now na kuwasha mtambo namba 7 wa bwawa la umeme letu.

Tupo busy na kuwasha treni ya umeme ya pekee kwenye nchi zote africa mashariki. Trilioni 16 zimewekwa pale.
Ambayo Rwanda itamchukua miaka 100 kuja kuipata
Rwanda hawana akili za kipuuzi kama hizi
 
Hii thread imenifanya nimkumbuke Mtikila R.I.P
 
Hapo naona uwanja wa Amahoro tu, ambao ni mdogo kuliko B. W. Mkapa
 
CCM imejimilikisha viwanja na kuwa kama kuku anaye tamia mayai hata kama yakiwa viza. Endapo viwanja hivi vingalirudishwa serikalini ilikuwa ni kazi rahisi sana kwa baadhi yake kujengwa tena upya ama kuvifanyia mabotesho makubwa ili vipate hadhi ya kimataifa.

CCM ni mzigo kwa taifa. Akili ndogo kamwe haiwezi kuleta matokeo makubwa na kwa wakati sahihi, Watawala wakijuacho ni ku "C&P" ili tu bora liende.
 
Back
Top Bottom