Kwa madaktari na wana JF wote ukisoma nipe dawa yake

Mtandaoni

Senior Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
132
Reaction score
64
Jaman wadau polen na majukumu ya siku ya leo wengine wanahitaji kupumzika walau akili itulie,

Kwa muda kama huu wapendwa wakati mmepumzika naomba mnitatulie tatizo hili.

Takriban wiki moja sasa nimekuwa nikisumbuliw na chembemoyo yaan inanifanya kukosa raha kwa sababu nasikia maumivu, naona chakula nilicho kula naona kingine kinabakia sehem panapouma, Madaktari mliopo humu naombeni mnisaidie nitumie dawa gan? Nisaidieni.
 
Pole mkuu majibu ya jamaa hapa chini yatakusaidia.

quote_icon.png
By Green gecko
Mkuu, "chembe ya moyo" ni maumivu ya sehemu ya juu ya tumbo (Epigastric pain) hiyo ni dalili ya magonjwa mbali yakiwemo ya kifua, moyo na tumbo. kwa watu wasio na elimu ya kitabibu wamekuwa wakifikiri kwamba ni ugonjwa unaojitegemea lakini sivyo. Ni sawa sawa na mtu anaekwambia kwamba anaumwa "homa" na akaenda kwa waganga wa kienyeji kutibu homa bila kujua ni ugonjwa upi unaleta hiyo homa.

Baadhi ya magonjwa yanayoambatana na chembe ya moyo (epigastric pain) ni haya hapa:
1. Magonjwa ya moyo (myocardial infarction etc.)
2. Vidonda vya tumbo (peptic ulcers)
3. varices
4. esophagitis
5. etc

Kwa maelezo google causes of "Epigastic pain" utaelimika zaidi

Kwa huyo mgonjwa wako mshauri aende hospitali apimwe ili aweze
 
Pole mkuu majibu ya jamaa hapa chini yatakusaidia.

quote_icon.png
By Green gecko
Mkuu, "chembe ya moyo" ni maumivu ya sehemu ya juu ya tumbo (Epigastric pain) hiyo ni dalili ya magonjwa mbali yakiwemo ya kifua, moyo na tumbo. kwa watu wasio na elimu ya kitabibu wamekuwa wakifikiri kwamba ni ugonjwa unaojitegemea lakini sivyo. Ni sawa sawa na mtu anaekwambia kwamba anaumwa "homa" na akaenda kwa waganga wa kienyeji kutibu homa bila kujua ni ugonjwa upi unaleta hiyo homa.

Baadhi ya magonjwa yanayoambatana na chembe ya moyo (epigastric pain) ni haya hapa:
1. Magonjwa ya moyo (myocardial infarction etc.)
2. Vidonda vya tumbo (peptic ulcers)

Asante mkuu utabidi nimuone doctor
 
Unapata maumivu wakati wa kumeza?unahisi chakula kimekwama kifuani?unacheua?unapaliwa?
 
Maumivu napta bt cio makali kivl ila nikimeza hata mate nahc kuna kitu kinazuia, kiungulia, kucheua ila cpaliwi nisaidie kwa hp.
 
Unatumia sigara au pombe? Kama ndio na hivyo ulivonieleza wahi upesi hospital
 
Back
Top Bottom