Kwa Madaktari naombeni tofauti hii!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Posts
11,483
Reaction score
3,369
Bila shaka WanaJF! Humu ndani tuna kila aina mtu humu. Naombe ni tofauti hii ktk hosptal zetu,tofauti kati ya Daktari na Mganga!
 
Sasa hapo ungeuliza jukwaa la lugha mpendwa!
Daktari ni kutohoa doctor, kiswahili sahihi ni tabibu (kwa maana anatibu)
Mganga nadhani anaganga, ila sijui tafauti
 
Bila shaka WanaJF! Humu ndani tuna kila aina mtu humu. Naombe ni tofauti hii ktk hosptal zetu,tofauti kati ya Daktari na Mganga!

... Hakuna tofauti kubwa katika hali ya kawaida,lakini kwa watumishi wa afya wenyewe hii inaonyesha grade ya mtu:
Kwa mfano kuna...
>>>daktari bingwa: huyu ni specialist.
>>>daktari: huyu ni lazima awe na degree ya chuo kikuu moja au zaidi ya Medicine...kidhungu anaitwa Medical Officer [M.O].
>>>daktari msaidizi au Assistant
Medical Officer [AMO]... Huyu anakuwa na Advance Diploma in Medicine.
>Mganga au Clinical Officer [C.O]... Huyu ana Ordinary Diploma ya Medicine.
>>> Mganga Msaidizi,Assistant Clinical Officer[ACO]... Huyu kitaaluma anakuwa amesomea cheti cha medicine.

.... Katika Makundi yote haya wanatofautiana kimajukumu na kiutalaamu. Ingawa M.O na A.M.O [madaktari] wanarandana katika baadhi ya majukumu... Vilevile pia kwa C.O na A.C.O [waganga].

... Hivyo ndivyo nijuavyo kwa upeo wangu mdogo...SATISFIED?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…