Kwa maisha wanayoishi ndugu zake Harmonize halafu nikimuona anatoa mil 9 kwa wengine, inaniuma sana

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Kwa wanaowafahamu ndugu zake na Konde boy Mtwara halafu Dogo akifika Dar anagawa Pesa kwa wengine inaniuma sana hata kama siyo ndugu zangu! Ingefaa dogo aanze kuwasaidia ndugu zake kwanza wote watoke kimaisha, ndipo umwage pesa ovyo ovyo kuliko kufanya hivi wakati ndugu zake walio wengi tunaowafahamu bado wanapambana na hali zao kwa kulima mhogo huko Mtwara

Kwa watu wa Mtwara mtaelewa ninachokisema na kukimaanisha hapa, tofauti na wanaume wa Dar
 
Mkuu kumsaidia mtu hata kama ni nduguyo si lazima ni hiari sasa wote wa mwangalie yeye kwa nini na wao wasijitahidi angalau wakatoka ki vingine? Nitamlaumu tu kama atakuwa kasahau mama basi
 
japo hana ulazima.. ila ajifunze kwa bosi wake...

diamond kasaidia wengi sana ndugu zake kuanzia esma, queen darleen, rommy jones wazaz wake pia.. pale WCB asilimia kubwa ya wafanyakazi nje muziki ni anaowajua toka tandale...

so Harmonize nae akumbuke jamaa zake na ndugu
 
Hata we we hiyo buku 2 ya bando unayotumia kufuatilia maisha ya wenzio kwenye mitandao ingeweza kabisa kumlisha mlo wa siku nzima au kununua panadol kwa ndugu yako huko kijijini kwenu.. So acha ujinga ishi maisha yako na upambane na halo yako.. Period!
 
MLACHAKE HANA AIBU. Hivi huyo harmony akitumia mali zake kadiri apendavyo kinawauma nn? Mbona wazungu 0wanatumia mamilioni kama watalii hamuoni ni shida? Kila mtu atumie mali zake apendavyo atoe zaka, sadaka, hisani msaada, atajua mwenyewe, je angekuwa maskini ungecomment huku? KUMBUKA MLACHAKE HANA AIBU.
 
Mkuu ungeweka bayana ndugu gani wa huyo kijana wanashida, kabla hujapandikiza chuki kwa wachangiaji.
Ni kweli mkuu...Mimi mwenyewe huyo
"Mayonnaise" ni mtoto wa shangazi lakini hajawahi kunipa hata mia mie nateseka hapa kijijini na biashara yangu ya majeneza.! Nilishamwambia anisaidie japo kupata masoko ya bidhaa zangu huko Dar lakn wapi.!
 
Kwa hizo pesa ulizopoteza kwenye michango ya harusi/club bora ungesaidia ndugu zako tu.
 
Ni kweli mkuu...Mimi mwenyewe huyo
"Mayonnaise" ni mtoto wa shangazi lakini hajawahi kunipa hata mia mie nateseka hapa kijijini na biashara yangu ya majeneza.! Nilishamwambia anisaidie japo kupata masoko ya bidhaa zangu huko Dar lakn wapi.!
Duuhhh! Pole sana
 
mkuu sidhani kama harmonize ana uwezo wa kugawa million 9. hiyo ni kiki am sure
 
HAJAMWAGA PESA,BALI AMETOA ZAWADI KWA RIDHAA NA FURAHA YA MOYO WAKE.
fuata hisia zako,tafuta pesa ,SAIDIA NDUGU ZAKO.
 
Nikuambie
Huwezi maliza umasikini wa uko hivyo ni haki kila mtu kupambana na hali yake
Rajabu namjua vizuri tena wote tunatoka mahuta chikongola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…