Kwa majukumu haya ya Tume ya Mipango, hivi mchawi wetu yuko wapi?

Kwa majukumu haya ya Tume ya Mipango, hivi mchawi wetu yuko wapi?

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
[h=2]katika pita pita yangu mitandaoni nimeona haya katika website ya tume ya mipango.

Roles and Functions of POPC[/h]1. To Develop Vision and Guidelines of the National Economy
2. Economic Policy, Economic Management and Research, National Development Planning Strategies.
• To assess the state of the National resources for developing and advice the Government on the efficient utilization of those resources,
• To analyse trends in the key Economic variables including balance of payments, money supply and prices and advises the Government accordingly,
• To analyse existing policies with the view to strengthen their implementation and to propose new policies where it is deemed necessary
• To monitor day-to-day performance of various sectors of the economy and ensure that appropriate measurers are taken to solve any operational problems as may be detected in those sectors,
• To ensure guidelines on economic relations with other states and international organization
• To develop National Demographic Strategies,
• To issue guidelines for the formulation of the National Plan and monitor the preparation process of long-term, medium-term and short-annual plans.
• To monitor the implementation of Government decisions on matters of planning and the management of the economy
• To analyse any social and economic issues and recommended to the Government appropriate policies and measures to be taken in the national interest

nashindwa kuelewa hivi mchawi kwetu sisi Tanzania yuko wapi?

tuna kitu kama hiki chenye malengo mazuri lakini hatutekelezi mradi wa kujenga uchumi mpaka iwe ni kutegemea miradi ya wafadhili.

tunajisema sisi ni nchi ya pili barani afrika kwa kufuga ngombe lakini tumeshindwa hata kuwapa wafugaji wetu soko karibu lote la ndani la maziwa tunajigamba kuwa na think tank .

tunazalisha matunda kwa wingi wananchi wetu wanakunywa kemikali kutoka asia kama juice na tunajigamba tunapambana na umasikini kutumia think tank.

tumeanzisha shirika la sido, limejikita katika kuzalisha bidhaa zisizokuwa sokoni kama bidhaa za mianzi, juice zenye imani pembeni na sio kutumia shirika hili kupunguza imports eti tuna think tank.

yapo mambo mengi mpaka unajiuliza hawa jamaa wanafanya nini?????

nachelea kusema yawezekana mifumo yetu inawafanya wasiweze kufanya kazi kwa maana makaratasi yanampa mamlaka haya lakini hali halisi ni kitu kingine.

ushauri wangu kwa raisi ajaye kama anataka kufanya kazi na baada ya miaka mitano ikawa ya tija, jambo la kwanza ni kuboresha tume hii.

ni bora tume hii ikahamishiwa kwa waziri mkuu kwa maana majukumu ya waziri mkuu kikatiba ndio hayo hayo ambayo ni kama yametafsiriwa kwa mapana katika majukumu ya tume ya mipango.

bila kuwa na mipango taifa haliwezi kupiga hatua kwa maana kwa sasa serikali inatumia gharama kubwa sana kufanya mambo yaleyale au kufanya mambo ambayo wakati wake bado.

jambo ambalo lingefanyika sehemu moja na kutoa huduma kwa serikali nzima unakuta kila wizara inafanya jambo lake, kila taasisi inafanya jambo lake.

mpango unaondaliwa na wizara moja unakwamishwa na wizara nyingine kutoplay part yake.
 
Ukienda pale utakuta wamekaa tu wanasoma magazeti. Kwanza hawajui wajibu wao, pili hawapewi fedha za kutekeleza kile wanachopanga kutekeleza.

Ndio maana JK aliamua kutengeneza taasisi nyingine inayoitwa presidential delivery beurau ili kutekeleza baadhi ya majukumu yao.
 
kimsingi ukiwa na vyombo viwili vinafanya kazi moja ni wazi kuwa chombo kimoja kitakufa na kingine ndicho kitasimama.

kuwa na tume ya mipango inafanya kazi zilezile kama za waziri mkuu na kuwa na waziri mkuu upande mwingine anafanya mambo hayo hayo ni wazi ama waziri mkuu atakuwepo kwa jina bila madaraka au tume itakuwepo bila madaraka.

vyombo viwili vinaweza kuwepo katika nchi zinazoendelea na vikafanya kazi iwapo watadefine mipaka ya kila mmoja lakini huku kwetu ni vigumu yaani ni sawa na mtu kuambiwa ukitunza kumbukumbu kwa komputa inasaidia biashara sasa muuza genge akadhani akiweka kompyuta kwenye biashara yake itakua.

kwa hali yetu vyombo hivi vitadhoofishana kwa maana lipo jambo atalifanya waziri mkuu kivyake na hawa hawana taarifa na wanaogopa kumuingilia kazi zake. yapo mambo raisi akiyapeleka tume waziri mkuu hawezi kuyasimamia.

kimsingi tume ya mipango ni chombo ambacho kinatakiwa kutafsiri sera katika action plan na kutathmini kinachondelea ili kubaini dira ya kesho. na hapa waziri mkuu anakuwa msemaji wa mambo ambayo yamefanyiwa kazi kitaalamu.

kama chombo hiki kinafanya kazi sio waziri yeyote kukurupuka na kuongea mawazo yake alafu ndio wataalamu waangalie wayatekeleze vipi na hapo akishayasema analinda kauli yake kuyatekeleza ili kulinda heshima yake hata kama ni waste kwa mustakabali wa nchi.

chombo hiki kama kinafanya kazi ndicho kinatoa mwongozo kwa wizara na wizara kufanyia kazi mwongozo na waziri au mwanasiasa yeyote anaenda kusema mambo ambayo wataalamu wake wamekwisha kamilisha na kuna mawasiliano na taasisi nyingine kupitia tume ya mipango kuhakikisha kila mdau amejiandaa.

lakini utampangia yule tu anayethamini umuhimu wa mipango.

kuna watu walikwisha ona umuhimu wa chombo hiki wakakiunda lakini hawakuweka mifumo ya kuhakikisha chombo hiki kinafanya kazi bali ni maamuzi ya viongozi. akija mwingine anaona kutumia fedha kupanga ni kupoteza fedha bila uende moja kwa moja kutekeleza chochote kinachokuja mbele yako anawanyima fedha.

ni bora tuweke utaratibu ambao mambo ya msingi tunayokwisha kubaliana si swala tena la kila anayekuja kufanya maamuzi yake juu ya hilo bali mfumo unamlazimisha kufuata utaratibu aliokuta na kama kitu ahakifai basi wapeleke mswada bungeni wawakilishi wa wananchi wajadili na kuamua na sio yeye kufanya maamuzi yake kupitia bajeti na mianya mingine.

Ukienda pale utakuta wamekaa tu wanasoma magazeti. Kwanza hawajui wajibu wao, pili hawapewi fedha za kutekeleza kile wanachopanga kutekeleza.

Ndio maana JK aliamua kutengeneza taasisi nyingine inayoitwa presidential delivery beurau ili kutekeleza baadhi ya majukumu yao.
 
Back
Top Bottom