Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Wanabodi hapa JF ninyi ni mashahidi jinsi wapinzani Tanzania walivyopinga utaratibu wa kisheria wa mtuhumiwa wa baadhi ya makosa ya jinai hasa uhujumu uchumi kuingia mkataba na DPP ili kukiri kisha kulipa na kurejesha walichokuwa wamewaponza watanzania.
Utaratibu huu ulipata baraka za Bunge la Tanzania. Kifungu cha 194 cha CPA kilifanyiwa marekebisho,na mtuhiwa wa makosa hasa jinai anaweza kuingia makubaliano na Dpp kisha kulipa kile acho hujumu.
Nia hasa ya kuleta huu utaratibu ni kuwezesha kesi kuisha kwa uharaka na kupunguza msongamano wa mahabusu gerezani. Lakini jambo ambalo wapinzani wa hapa Tanzania walikengeuka na kuanza kueneza uongo kuwa huu utaratibu umewekwa ili kumnufaisha DPP.
Maneno na porojo nyingi zimetangazwa hapa Tanzania. Mara DPP amepewa mtaji wa kujinuisha,mara huu utaratibu wa kisheria umewekwa kuwakamua wapinzani na wakosoaji wa serikali iliyipo madarakani.
Leo hii kuna gazeti la hapa Tanzania limetoa takwimu kuwa Bil 123.6 zimekusanywa kupitia ofisi ya DPP. Hii ni habari njema sababu pesa hizi zimekusanywa kwa mujibu wa sheria. Na nia kuu ni kuhakikisha waliofanya makosa hawakai rumande muda mrefu,huku magereza yakipumua maana mrundikano wa wafungwa na mahabusu ni mkubwa.
Oni langu, wapinzani msiwe mnakurupuka kupinga kila kitu kisa tu mnatafuta kick kwa wanachi.