Uchaguzi 2020 Kwa mapokezi makubwa anayoyapata Lissu, chondechonde nawaomba NEC na Vyombo vyote vya Dola

Hebu acha KUKURUPUKA na KUROPOKA UJINGA! Aliyekudanganya hii picha ni ya fisadi lowassa ni nani?

Niweke picha ya fisadi lowassa ili iweje?
😳😳😳


Mkuu, na picha za 2015 zinahusikaje hapa tena?

Tuongezeni juhudi ya Kampeni na kuhamasisha watu ili tuondokane na aibu ya kutumua picha na video za nyomi ya Lowasa
 
Wengi washangaaji tu, Lissu uwezo wa kuongoza nchi hana, CHADEMA ni dhahifu sana na ikitokea siku wakaongoza watakuwa mafisadi wakubwa sana, walionesha madhaufu yao makubwa sana 2015
Huu ndio ukweli, kwa watu waonao mbali.
 
Nafurahi kwa kuwa umekubaliana na mimi kwamba hakuna demokrasia nchini,kwa kisingizio kuwa ni mpango wa mataifa ya magharibi. Kama ndivyo hatuna haja ya kufanya maigizo haya ya uwepo wa vyama vingi vya siasa kama ninyi mnaamini kuwa demokrasia inaleta umaskini.
Lakini ukumbuke hizo nchi za magharibi ndizo zenye maendeleo japokuwa wana demokrasia nzuri!! Wewe umeirejea nchi gani kusema kuwa demokrasia inaleta umaskini?
 
Umesema kweli mkuu ila Kuna jamaa yangu mjeda anakuambia vijana wengi walioko jeshini intake mpya mpya wanapenda haki na mabadiliko sasa sielewi anamaanisha nini.
😂😂😂 Eti vijana wengi..? Ubaya Ni kwamba higher officers kwenye vitengo mbalimbali jeshini, kwa asilimia kubwa Ni wafuasi lialia wa CCM, na Marafiki wa huyo mnaemuita jiwe na masirahi yao Ni makubwa kuliko mnavyofikiri(hawana njaa).Ni ngumu Sana kulitumainia jeshi hapa TZ, hasa kwa mfumo huu wa uongozi ambao rais Ni Amri jeshi mkuu.
 
Sawa Mkuu! Kwa hiyo msimamo wako ni upi Kati haya mawili?
1. Kuwa na chama kimoja cha siasa.(chama dola)
2. Kuwa na vyama vingi vya siasa kama tulivyo Sasa?
Ni kweli wazungu walitutawala na bado wanaendelea kututawala hata sasa. Unataka kuniaminisha kuwa yote wazungu waliyowafanyia babu zetu ni mabaya? Tuongee tuongeavyo,demokrasia ni Jambo muhimu sana katika jamii,kwa maana ya majority rule, wengi wape. Tofauti na hapo unasababisha huzuni na kusinyaa kwa mioyo ya wengi. Siku watakapompata mtu wa kuwasemea na kuwaongoza kwenye nini cha kufanya pale ambapo haki haitendeki ndipo tutakapoanza kulalamika kuwa ni hila za watu wa magharibi,wakati kumbe hata hawahusiki.
Demokrasia na haki huzaa amani. Vinginevyo ni kuendelea kujikusanyia kuni wenyewe huku tukimsubiri wa kuziwasha moto.
 

KURA ZINAPIGWA NA WANAICHI MAAMUZI WANAFANYWA NA USALAMA WA TAIFA NA WATU WACHACHE SANA.... MNAJISUMBUA
 
Mnataka demokrasia gani nyie watu🤔?
Amini nakwambieni, kwa nature ya watanzania demokrasia ikiendekezwa sana, hatutapiga hatua.Hiki kiwango Cha demokrasia kinatosha Sana.
Duh! Unatumia ushahidi gani kusema tukitumia demokrasia hatutapiga hatua? Acheni kuingizwa mkenge na waroho wa madaraka. Kila pambio wanaloimba mnadakia tu, vinginevyo na wewe labda ni mnufaika wa udikteta uchwara ndiyo maana unatetea huu ubakaji wa demokrasia.
 
Duh! Nilidhani napeana changamoto na mtu mvumilivu kisiasa,kumbe sivyo. Pole Mkuu, maana nikiendelea zaidi naona dalili za kukoseana heshima. Nakubali kutokukubaliana nawe.
 
Chadema ni watu wa ajabu sana, kama kawaida yao kujaza kwenye kampeni lakini kwenye uchaguzi mnaambulia maumivu tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…