che wa Tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2011
- 277
- 71
Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika aina za VIRAI/VIKUNDI. Mfano mwandishi James Mdee ana aina mbili tu yaani Vikundi Nomino na Vikundi Vielezi, Oxford university press wao wana kirai nomino,kirai kitenzi, kirai kivumishi na kirai kielezi, Taasisi ya ukuzaji mitaala wao wana aina tatu za virai, virai jina, virai vielezi na virai vivumishi, Mbunda msokile mawazo yake yapo sawa na james mdee nae ana aina mbili tu za virai yaani virai nomino na virai vielezi. Upi ni mchanganuo sahihi wa aina za virai?