Kwa mara Nyingine tena Nimechunguza uwiano wa bando nalolipia na matumizi halisi niliyotumia kwa mwezi, ungana nami katika matokeo ya Research

Hii ikoje mkuu? Hebu tufahamishe vizuri.
Ni postpaid ya airtel ukiungwa unajiunga hata kama una pesa unajiunga siku nyingine ila vya tigo ukiungwa usipo lipa wanakula kichwa yaani wanakuzimia laini au unaekewa deni
 
Ni postpaid ya airtel ukiungwa unajiunga hata kama una pesa unajiunga siku nyingine ila vya tigo ukiungwa usipo lipa wanakula kichwa yaani wanakuzimia laini au unaekewa deni
Airtel wanaita sme
 
Ila hawa Tigo kuna siku nilitumia 4GB bando lote nililokua nimejiunga, kuja kucheki data Usage kwenye simu ilikua inasoma 4.35GB kama sijasahau, nikahisi labda walisahau make ilikua speed sana, 5MBps.
NB: Nilikua napakua ROM ya simu.
 
Gb 30 na sitoboagi mwezi. Tar 28-30 ngoma inakata.
Basi hao jamaa ni wezi zaidi ya hawa hapa wa HALOTEL. Tazama 25% ya data ilivyofywekwa ndani ya dakika 2 tu? Hawa majamaa ni wezi hadi wamepitiliza aisee:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…