kilambimkwidu
JF-Expert Member
- Jul 21, 2017
- 6,097
- 7,199
Ndugu wana Chit-Chat,
Tangu nimeijua dunia sijawahi kuvaa vazi la suti, hua naona watu tu wamevaa. Inasemekana ni vazi rasmi kwa shughuli maalum kama harusi. Mimi zangu ni: chini sandoz, suruali kadeti/jeans/kodrai na tisheti hasahasa tisheti ya jezi au shati ya mikono mifupi, basi. Sijawahi kuvaa suti wala hata tu kuchomekea suruali na shati sijawahi. Na hata shati la mikono mirefu kwangu ni mwiko.
Ninao mtihani siku ya harusi ya dada mwezi wa kumi. Jana kenye kikao cha familia kaka wa bibi harusi nimeamrishwa kuvaa suti siku hiyo. Naambiwa imetengwa hela nikashoneshe suti na nimeambiwa rangi nichague mwenyewe. Sina ujanja, imebidi nikubaliane na jambo hilo.
Nafahamu hapa kuna wataalamu wa mitindo na wenye uzoefu na vazi hili. Naomba ushauri wenu kuhusu mambo ya kuzingatia ninaposhonesha hiyo suti ili fundi asiniharibie nguo. Pia nawaza, je ni dizaini gani ya suti inaweza kunifaa na mwonekano wangu siku hiyo utakuwaje?
Kama kuna mtu alivaa akapendeza naomba unisaidie picha ya fashion yake ili nimpelekee fundi wangu ageze mshono huo. Mimi ni mrefu futi 5 na ni mweusi.
Natanguliza shukrani.
Sent using Jamii Forums mobile app