Kwa Marekebisho haya ya Canon Laws( jus canonicum), Sister Susan Bathlomeo anayedaiwa kujiua afanyiwe ibada na heshima zote!

Mkuu mbona wewe kwa uelewa wako haukutakiwa kuuliza Swali Illogical Kama Hili?
Unaweza kuona swali illogical kama huelewi logic ni nini.

Ndiyo maana huelewi swali, na kwa kufuatia, huelewi jibu wala muunganiko wa swali na jibu.

Hutakiwi kusema ukifuata mlolongo wa kanisa hakuna litakaloharibika wakati kuna watu kibao wanakwenda kanisani na wanaishia kubakwa humo kanisani.

Tena kanisa Katoliki hilo hilo.
 
Mkuu embu nieleze unaielewaje Logic? huenda una maana yako (Mimi naielewa Logic kimahesabu na Kifalsafa)
 
Mkuu embu nieleze unaielewaje Logic? huenda una maana yako (Mimi naielewa Logic kimahesabu na Kifalsafa)
Logic hiyohiyoya kimahesabu na kifalsafa inakataza kuahidi kitu usichoweza kutimiza.

Kauli yako inalifanya kanisa liahidi kitu lisichoweza kutimiza.
 
Ibada za Mazishi mara nyingi si kwa ajili ya Marehemu, Zipo kwa ajili ya kuwakumbusha wakrsitu walio hai umuhimu wa kuishi katika kushikamana na kanisa

Aksante mkuu ila kule kwetu huwa tunaenda kuandikisha misa za kuwaombea marehemu na pia huwa tunaenda kumchukua Padre aje kutusomea misa ya marehemu ili tumuombee kwa Mungu. Mungu amsamehe makosa yake na ampokee kwenye Raha ya milele.
 
Logic hiyohiyoya kimahesabu na kifalsafa inakataza kuahidi kitu usichoweza kutimiza.

Kauli yako inalifanya kanisa liahidi kitu lisichoweza kutimiza.
Hitaji la watu sio Kutokufa Hili najua waelewa Mkuu Kiranga, hitaji la watu wengi ni Marehemu au ndugu au jamaa zao waliofikwa na Msiba waweze kupata Huduma ya Misa za Mazishi kutoka kwa uongozi wa kanisa! na Kanisa halina ahadi kama hiyo ya kuahidi kutokufa!
 
Aksante mkuu ila kule kwetu huwa tunaenda kuandikisha misa za kuwaombea marehemu na pia huwa tunaenda kumchukua Padre aje kutusomea misa ya marehemu ili tumuombee kwa Mungu. Mungu amsamehe makosa yake na ampokee kwenye Raha ya milele.
Hiyo ipo, Hata kwenye nia za Misa huwa inawekwa na kusemwa kabla ya ibada kuanza
 
Umewauliza watu wangapi kati ya mabilioni ya waliokufa kwamba hawakutaka kuishi bila kufa, angalau walivyokufa tu, wakakuambia hawakuwa na hitaji la kutokufa?

Na kama unajua kanisa halina ahadi ya kutokufa, utasemaje mahitaji ya watu hayata haribika wakifuata kanisa?

Huoni kwamba unawalaghai wasiotaka kufa kwa kuwapa matangazo ya biashara ya uongo kwamba mahitaji yao hayataharibika, kabla hata kuwauliza mahitaji yao ni yepi?

Wakikwambia mahitaji yao ni kutokufa je? Bado utawaambia wafuate kanisa na mahitaji hayo ya kutokufa hayataharibika?
 
Kati ya CIC na CCC which one takes the upper hand? Bila kusahau Magisterium katika muktadha huu!

CHAPTER II: THOSE TO WHOM CHURCH FUNERALS ARE TO BE ALLOWED OR DENIED
Can. 1183 §1: As far as funeral rites are concerned, catechumens are to be reckoned among Christ’s faithful.

§2 Children whose parents had intended to have them baptized, but who died before baptism, may be allowed Church funeral rites by the local Ordinary.

§3 Provided their own minister is not available, baptised persons belonging to a non-Catholic Church or ecclesial community may, in accordance with the prudent judgement of the local Ordinary, be allowed Church funeral rites, unless it is established that they did not wish this.

Can. 1184 §1 Church funeral rites are to be denied to the following, unless they gave some signs of repentance before death:
1° notorious apostates, heretics and schismatics;
2° those who for anti-Christian motives chose that their bodies be cremated;
3° other manifest sinners to whom a Church funeral could not be granted without public scandal to the faithful.

§2 If any doubt occurs, the local Ordinary is to be consulted and his judgement followed.

Can. 1185: Any form of funeral Mass is also to be denied to a person who has been excluded from a Church funeral.
 
Kwanza kabisa watu wengi wenye akili timamu hufahamu kuwa kifo ni lazima lazima ufe tu kwa maana hiyo hakuna excuse ya kufa, Ninaposepa mahitaji ya watu hayatoharibika usiniMisquote, Namaanisha mahitaji ya watu kadri ya yale ambayo hutolewa na Kanisa!
Hapa Nafikiri umenielewa!
 
Kwa nini kifokiwe lazima kama kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote?

Huyo Mungu anapenda sana kutenganisha watu na familia zao?

Anapenda sana kuona watu wanalia kwenye misiba?

Ameshindwa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?
 
Kwa nini kifokiwe lazima kama kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote?

Huyo Mungu anapenda sana kutenganisha watu na familia zao?

Anapenda sana kuona watu wanalia kwenye misiba?
Umeuliza swali Ambalo kwenye Mada yangu Sikulilenga!
 
Huyo Mungu anapenda sana kutenganisha watu na familia zao?
Lengo la Mungu halikuwa Mtu Kufa at first, ila baada ya wazazi wetu wa kwanza kutenda dhambi Mungu akawapa adhabu ya kifo wao Pamoja na uzao wao wote..
 
Lengo la Mungu halikuwa Mtu Kufa at first, ila baada ya wazazi wetu wa kwanza kutenda dhambi Mungu akawapa adhabu ya kifo wao Pamoja na uzao wao wote..
Hujajibu swali langu, Mungu alishindwakuumba ulimwengu ambao kifohakiwezekani kabisa?
 
Hujajibu swali langu, Mungu alishindwakuumba ulimwengu ambao kifohakiwezekani kabisa?
Mkuu usikaze kichwa hilo swali nimekwisha kulijibu soma vizuri
 
Mkuu usikaze kichwa hilo swali nimekwisha kulijibu soma vizuri
Nimekuuliza swali moja, ulilojibu wewe jingine.

Mimi nimekuuliza, kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kabisa, hata kitokee chochote kile?

Wewe unanijibu kifo hakikuwa mpango wa Mungu,ila blah blah.

Ukishaweka "ila blah blah" tu, maana yake Mungu hakuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kwa hali yoyote ile.

What do you mean? Mungu hakutaka ulimwengu uwe na kifo, ila kifo kikampiga Mungu chenga ya mwili kikaweza kuwepo bila Mungu kukusudia? Mungu alilala usingizi kifo kikapenya bila yeye kutaka?

Sasa hujajibu swali langu.

Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezi kutokea kwa sababu yoyote ile?

Aliogopa dunia itajaza watu na atashindwa kuwapa watu nafasi ya kukaa?
 
Ndiyo
 
Mimi nimekuuliza, kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kabisa, hata kitokee chochote kile?
Mkuu wewe sio mtaalamu wa kusoma na kuelewa vifungu, Mungu aliwaumba watu wasife Milele na Milele (ndivyo dhamiri yake ilivyokuwa) hawa watu wakatenda dhambi ( na kwa kuwa Mungu ana uwezo wa kutengua Jambo lake alilolifanya akatengua na akawapa adhabu ya kifo)
 
Kama Mungu aliwaumba watu wasife milele na milele, na hiyo ndiyo ilikuwa dhamiri yake.

Halafu ikaja kutokea watu wameweza kufa, kwa sababu yoyote.

Huyo Mungu ameshindwa kutimiza alichotaka kufanya.

Na kama kashindwa kutimiza alichotaka kufanya, huyu si Mungu muweza yote.

Alitaka watu waishi milele bila kufa, akashindwa kutimiza hilo.

Unaelewa hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…