Kwa maslahi mapana ya wasio na ajira rasmi

Kwa maslahi mapana ya wasio na ajira rasmi

Barnabas Mashamba

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2020
Posts
797
Reaction score
2,233
Ndugu wanaJF

Nimeona nishirikishe wasio na ajira rasmi kazi nitakayoieleza kwa mapana katika uzi huu (kwa vitendo kuanzia ufanyaji wa hali ya chini (kiwango duni) hadi kiwango cha juu) huku tukisubiri mirija ya asali (kazi tulizoomba) ifunguke.

Ndugu wanaJF

Natambua kuna fursa nyingi sana mtaani, kuna zinazohitaji mitaji na zinazohitaji uthubutu wako tu (hata kama huna mtaji). Hapa nitakuletea fursa ambayo unaweza ifanya hata kama huna mtaji ila una uthubutu pekee.

Ndugu wanaJF

Fursa yenyewe ni upigaji wa picha kwenye matukio mbalimbali (sherehe, mahafali n.k).

Ndugu wanaJF

Kwa kuanzia, leo darasa la saba wanahitimisha elimu yao ya hatua ya msingi ili mwakani waendelee na elimu ya upili (sekondari), sasa hiyo ni pesa.

Ndugu wanaJF

Kwa hali ya chini kabisa, ili uweze kupiga picha kwa wanafunzi wapate kumbukumbu za siku hii, unahitaji uwe na smartphone, kuna mtu anajiuliza, mbona huo tayari ni mtaji, kama sina smartphone huoni itanihitaji niwe na pesa ya kununua smartphone kwanza?

Ndugu mwanaJF

Namna ya kupata kifaa cha kupigia picha (kama huna ama kamera au smartphone) fanya yafuatayo.
1. Azima smartphone ya ama rafiki yako au ndugu aliye karibu, au mwanakanisa au mwanamziki mwenzako. Mweleze unaenda kufanyia nini, utapata.
2. Nenda kwenye photo studio iliyokaribu nawe na uulize swali hili "wapi nitapata kamera ya kukodi", utaelekezwa.

Ukishapata kifaa elekea sehemu ya tukio (shuleni) mida ambayo wanafunzi wanamaliza mtihani (around saa 10), kama una kamera ivae shingoni na mchezo utaanzia hapo. Kama una smartphone, utahitajika kuwatangazia wanafunzi kuwa unapiga picha.

Saa kumi nitaleta update humu ya namna mimi binafsi nitakavyokuwa nimeandaa eneo la kupigia picha.

Usisahau hili, piga picha chukua pesa, usipochukua pesa nakuhakikishia kuna picha utasafisha na hazitalipiwa (no matter how good they appear), kuna wanafunzi wanapiga kujifurahisha tu. Hivyo ukipiga picha na kuchukua pesa itakurahishia kwenye zoezi la kusafisha picha (means utasafisha tu zile zilizolipwa).
 
Ndugu wanaJF, msimuwekee kabisa maanani huyu mtoa mada! Maana yeye mwenyewe anaishi maisha ya kichawa! Sasa hiyo nguvu ya kuwashauri nyinyi kujiajiri, anaitoa wapi?

Ndugu wanaJF, fanyeni kama mnampuuza tu huyu mtoa mada. Kwa sababu hana jipya la kuwaeleza. Yeye anachojua ni kumsifia tu yule bosi wake anayetutesa na tozo kandamizi.
 
Set up yangu kwa leo ilikuwa ifuatavyo.

IMG_20221006_172134_622.jpg


Zoezi la uchukuaji picha lilianza around saa 10 jioni. Kulikuwa na break mbili, ya kwanza pale wanafunzi walipotakiwa kwenda kisimani kuteka maji ya kuoshea sahani walizotumia kula chakula. Awamu ya pili ni pale lilipokuwa na mazungumzo kati ya mwalimu mkuu na wanafunzi.

Zoezi liliendelea hadi jua lilipozama (pale simu ilipokosa uwezo wa kupiga clear photos), kwa maombi waliyofanya wanafunzi, zoezi nitaendelea nalo asubuhi ya kesho.

Ili kupata picha nyingi zaidi, nilimuomba mwalimu mkuu kupiga picha na wanafunzi waliotaka picha ya ukumbusho na yeye, hapa credit nampa mwalimu mkuu na mwalimu aliyekuja baadaye, maana picha ziliongezeka zaidi kwa idadi tofauti na zile za wanafunzi pekee.

Naamini kama kuna mtu (jobless) amefuata hii, hatakuwa amekosa kiwango cha chini cha 50,000/= (hii ni kwa kuwa idadi ya wahitimu inatofautiana kati ya shule moja na nyingine).

Kwa kuwa wanafunzi wamehitimu, kesho nitakuja na nini cha kufanya kuendeleza na hivyo kuendelea kugonga hela.

Barnabas Mashamba
Future Phd (Mathematics) holder

Quote: It is a daily routine that makes a difference.
 
Back
Top Bottom