Asante kwa uzi huu mkuu. Nahitaji kununua gari dogo kwa matumizi ya kawaida/mizunguko ya mjini na masafa ya mkoa kwa mkoa. Vipi kuhusu "Aud"?
Asante kw swali, ingawa gumu kweli; sio kw kujibu ila kwa kujibiwa!
Kwa hilo swali lako kuna contradicting factors mbili ambazo kuafikiana ni mbinde! 'Gari dogo' la matumizi ya mjini haliwezi kua nafuu kwa 'masafa ya mikoani' ILA kwa miundo chache kama "AUDI" (ulivyotaja) Benz na magari/miundo michache ilyo na 'the right mix' ya 'Sport- Touring' (GT) na economy. Magari haya yanahitaji matunzo ya hali ya juu na pia uangalifu flani; SIO KUSEMA GHALI! Linalotatiza zaidi ni uelewa - kwanza wa mwenye gari, THEN ujuzi wa fundi - nasema hivi sababu ukipata gari la kifahari linakarabatiwa kichochoroni, kwanza kaamua mwenyewe kisha kampa fundi PERIOD
La kuzingatiwa kimsingi (kando na magari tulioangalia hapo juu), ni kua matumizi ya mjini yanahitaji engine ndogo, na kw hivyo uzito mdogo wa gari ilhali kwa safari za mikoani inafaidi kua na gari kubwa ili kua na inertia/momentum ya kuwezesha cruising - mzunguko mdogo wa engine kw kudumisha kasi ya gari!
Magari ya kisasa yana teknolojia zinazowezesha mashine kubwa kutumia mafuta kidogo kama vile VVTI, CGI, D4/8, VTEC, n.k. na pia mashine mdogo kua na nguvu zaidi kw kutumia turbo za VNT/VG, n.k.
Kuna factors zingine pia za kibinafsi itabidi uangazie kw makini ili kupata suluhu. Mambo kama ukubwa wa familia(idadi ya abiria), mazingira ya matumizi hasaa kw safari (Off au On-tarmac), upatikanaji wa utaalam na spare na pia kimo cha mfuko na/au upana wa mawazo yako!
La kuwaza! Aliye na Patrol 4.2 hulsusan safari za mikoani na pia Isis au Toyota/Nissan nyingine ndogo kw matumizi ya mjini, anatumia hela kidogo kw magari hayo zaidi ya aliye na lake moja na PIA baada ya mda kudhoofika kw body na mashine kutapunguza resale value ya hii asset muhimu!
Na kwa hayo yangu machache, maamuzi ni kwako kaka ila ijapo kuna swali, by all means .....