Habari za masiku wanaJF,
Kwa mda flani sasa nimekua nikifatilia swala la matatizo ya magari, na vyombo vya moto kwa jumla hapa, kwa sababu za kutoa ushauri - sio kw malipo, na pia huduma - kw mapatano.
Hapa naanzia uzi wa kutoa msaada wa mawaidha, utakavyofanya au fatilia tatizo ili uelewe utakavyotatua na kujibu maswali yoyote kuhusu ufundi wa magari na vyombo vya moto.
Napendekeza kuweka issue/tatizo hapa kwa forum ili wengine waeze kusaidika ILA kuna mambo yatabidi tuyagange nyuma ya pazia.
So, karibuni nyote.
Mkuu kuna uwezekano wowote nikapata operation manual ya toyota succeed iliyoandikwa kwa kiingereza?Muunda gari/chombo hua ameandika kwenye owner/operator manual au/na kwenye mfuniko wa chupa pale kw master cylinder. Ni muhimu kuzingatia
Shukrani mkuu nikifanikiwa kulitia mikononi ndinga nitakupa mrejeshoAsante kw swali kaka,
Uamuzi mzuri huo!
Toyota Crown Athlete ni dinga poa sana ya daraja la executive models. Engine yake ni ya piston sita na inauwezo tosha wa kuibeba ile body kw kasi/nguvu inayofaa. Engine za sasa hazina issue kibao ila makini kw matunzo, spare na matumizi. Hakikisha oil ni synthetic pekee, spare ni genuine na fundi anaielewa gari na mifumo ya kisasa...
Habari, sijui utakuwa una ifahamu hii cheapest full synthetic oil nimekuwa nikiitumia kwa muda sasa kwenye injini ya 1kr-fe lakini changamoto ni oil kuisha sana na kwakweli hakuna sign ya leakage japo kidogo huwa kuna moshi blue labda gari ikiwa katika very high revolution, sasa cjui ni oil nzuri? View attachment 888230
Hilo ni tatizo la solenoid hiyo ya pressure inayopunguza pressure wakati wa engagement toka P au N na pia wakati mwingine kwenye D. Yakaa tatizo lenyewe ni intermittent kw kua lapotea unapofanya Key Off reset. Fanyiwa uchunguzi upande wa circuit/wiring kabla ya kuibadili solenoid yenyewe.Natafuta fundi wa gari (Mazda DEMIO 2003), kwenye dashboard inablink neno "HOLD" hii ni baada ya kuwa gari injini imepoa vya kutosha, na ukihamisha gia hasa kwenda kwenye R,inagonga sana (kama inastua) gari inakuwa nzito ila ikitembea kilometa kadhaa ukaizima na kisha kuiwasha hilo neno HOLD linatoweka na gari inakuwa vizuri, baada ya kufanya diagnosis nikapata majibu ya code: P0745 EPC Circuit Fault. Baada ya kugoogle hilo tatizo nikakuta ni tatizo la Control Solenoids hasa " Pressure Conrol Solenoid) ambazo ziko kwenye GIA BOX. Naomba kama kuna mtaalam anaweza tatua hili tatizo tuwasiliane.
Hilo ni tatizo la solenoid hiyo ya pressure inayopunguza pressure wakati wa engagement toka P au N na pia wakati mwingine kwenye D. Yakaa tatizo lenyewe ni intermittent kw kua lapotea unapofanya Key Off reset. Fanyiwa uchunguzi upande wa circuit/wiring kabla ya kuibadili solenoid yenyewe.
Ahsante sana kwa ushauri Mkuu, nilibadilidili plugs kwa kuagiza kupitia agent wa Toyota bt tatizo liliendelea kuwepo pia kuna fundi alinichekia akadai tatizo liko kwenye Air Mass flow imechafuka aliposafisha tatizo liliisha baada ya muda likajirudia. Naomba ushauri wako zaidiHapa issue yaweza kua tuning, plugs zisizoifaa engine au kasoro/tatizo kw mfumo wa VVTI. Diagnosis kwanza.
Ahsante sana kwa ushauri Mkuu, nilibadilidili plugs kwa kuagiza kupitia agent wa Toyota bt tatizo liliendelea kuwepo pia kuna fundi alinichekia akadai tatizo liko kwenye Air Mass flow imechafuka aliposafisha tatizo liliisha baada ya muda likajirudia. Naomba ushauri wako zaidi
Nimerudi mkuu nilipitia engen yote haina leakage kabisa,wakati wa service nilibali oil ya engen ikipungua kwa litre nzima,Ni wazi kua ile issue ya vacuum kuwa juu na kuvuta oili kw manifold haiko. Oili yaweza kua yatokea kwa gaskets au seal, fanya engine wash ya nguvu kisha ukague engine kw makini.
Kuna rafiki yangu ana Harrrier old model engine 2990cc anataka kuibadilisha na kuweka engine ya harrier hybreed 2400cc. Jee itabidi abadilishe na gearbox?Asante kwa maelezo.
Mkuu hii kitu niliipata katika raum yangu lakini niligundua ukiendesha pasipo kufunga mkanda hiyo Alama inaonekana. Jaribu kufunga mkanda then tupe mrejesho hapa jukwaaniMkuu, asante sana kwa ushauri unaotoa hapa jukwaani
Swali langu ni je una maelezo yoyote kuhusu taa ya pembe tatu na alama ya mshanga ndani mwake inayowaka katika gari za toyota raum??! maana mwanzo nilidhani ni yangu tu ila nimefatilia kila raum inawaka hiyo taa hata kama imetoka japan jana, je technical problem toka kiwandani ama ni nini hasa!!!! Gari haisumbui
Pili, ni ATF ipi nzuri inayofaa kutumika kwenye raum??
Sio aipime mwenyewe ?? Kama bado haja lekebisha na yupo dar mm nampa ofa ya kumpimia bureee kabisa na mashine za kutosha kuanzia TIS launch pro3 autoboss v30.maxidas ,ucandas n.k but kwa kufika ofisini lkn kama atataka kufuatwa alipo basi garama yake itakuwa ni kulipa usafiri tuu basi.Vipi kaka
Unahitaji kufanyiwa diagnosis vizuri ili kuisoma hiyo code iliyoashiriwa na taa. Karibu umtafute fundi ana Techstream au uende kw Toyota Tanzania waifanyie diagnosis.
Mkuu kama nimekuelewa basi hilo swala ni gumu sanaaa aachane nalo nigum sana garama zake ni bora akanunua gari yenye mfumo huo wa hybrid..Kuna rafiki yangu ana Harrrier old model engine 2990cc anataka kuibadilisha na kuweka engine ya harrier hybreed 2400cc. Jee itabidi abadilishe na gearbox?
Ahsante sana kwa ushauriSio aipime mwenyewe ?? Kama bado haja lekebisha na yupo dar mm nampa ofa ya kumpimia bureee kabisa na mashine za kutosha kuanzia TIS launch pro3 autoboss v30.maxidas ,ucandas n.k but kwa kufika ofisini lkn kama atataka kufuatwa alipo basi garama yake itakuwa ni kulipa usafiri tuu basi.