Kwa matatizo ya gari

Battery kuisha yaashiria short au matumizi ya moto gari likiwa limezima. Lazima iangaliwe ni kitu kipi kinakula moto gari likiwa off.
Hydraulic oil iliyo pendekezwa ni ile ya Toyota au waweza timia ya Total Fluid IID
 
Gari yangu gx 115 ikitembea umbali wa kilomita kama 20 ivi inawasha chek engine notification
 
Mi naulizia tairi za za size gani zafaa kunyanyulia Toyota Raum new model ya 2005. Na nawezapata kwa shilingi ngapi.
Kuinyanyua gari sio jambo rahisi hivyo sababu ya usalama/ustadi barabarani. Ni vyema kushughulikia springs sababu hizo ndio hua zimeisha.
 
Gari yangu gx 115 ikitembea umbali wa kilomita kama 20 ivi inawasha chek engine notification
Yadai diagnosis kaka ili kubaini tatizo. Haitakufaidi na itakuogofya bure kukisia tatizo kabla diagnosis. Kulingana na maelezo yako nashuku upande wa mafuta na emissions - sio jambo la kutishia.
 
Mkuu heshima kwako...nina swali ambalo huenda litatoa majibu kwa wengi. Kuna athari yoyote ya kiufundi kwenye gari endapo nitaamua kuondoa catalytic converter endapo imekuwa clogged?

Je, athari za kuiondoa kabisa ni zipi kwa sababu kifanya replacement nadhani itakuwa ni gharama kubwa.
 
mkuuu nina gari yangu mistubish rosa 4d 33 .ni daladala tatizo lake.asubuhi ukiiwasha inakubali kabisa na unapiga kazi vizuri tu lakini baada ya ruti moja au mbili gari ikipumzika standi kusubiri abiria.

Wakati ushapakia abiria ukiiwasha huwa haikubali kuwaka mpaka isukumwe.au ukijaribu kuiwasha na kupandisha mafuta mara moja moja huwa inakubali..nimewajaribu mafundi kila mmoja anasema lake sasa mkuu naomba msaada wako.
 
Kw gari ya petroli haina madhara mengi kw gari ila mwongezeko wa moshi kw mazingira. Magari ya diesel yenye mfumo wa DPF ndio yana issue kidodo sababu mfumo ni 'closed loop', yaani kuna taarifa zitokako kw ile DPF filter/muffler kurudi kw kompyuta.
 
Hii lazima iangaliwe kw jaribu sio kukisia kw mbali
 
Hili litakua tatizo upande wa umeme hasa kw mfumo wa engine idle stabilization. Itakua vyema ukifanya tune-up ya uhakika na pia diagnosis ya engine, gearbox na mfumo wa umeme in general.
Nina toyota Cami nataka kuifumua system yote ya umeme na kuiweka sawa/upya.. inaweza kugharimu kiasi gani, ufundi na vifaa?
 
Styvo254 Gari yangu RAV4 - kill time nikisimama hasa kwenye folen inatetemeka bodi lote nikitembea inatulia, nikiwasha AC inatetemeka zaidi, nikiweka parking inapunguza mtetemo. shida inaweza kuwa nini? naweza pata mtaaalamu? maana nishaonana na mafundi wengi lakini haiponi.
 
Daa pole...mimi siyo fundi ila hapo nakushauri anza na zoezi rahisi la kuangalia engine mounts na gear box mounts.....hizi bush zikichoka huchangia hilo tatizo..
Kama ziko poa waone wataamu zaidi wa vipimo.
 
Daa pole...mimi siyo fundi ila hapo nakushauri anza na zoezi rahisi la kuangalia engine mounts na gear box mounts.....hizi bush zikichoka huchangia hilo tatizo..
Kama ziko poa waone wataamu zaidi wa vipimo.
Asante mkuu. Hizo zote nishafanya na nikafunga mpya (original) zote.
 
Asante mkuu. Hizo zote nishafanya na nikafunga mpya (original) zote.
mkuu unaposema mpya ni za dukani au used? nami zilikata mbili nikanunua mpya dukani kufunga gari ilikuwa inatetema na body nikatoa nikatafuta used za Japan ikatulia.
 
mkuu unaposema mpya ni za dukani au used? nami zilikata mbili nikanunua mpya dukani kufunga gari ilikuwa inatetema na body nikatoa nikatafuta used za Japan ikatulia.
Hata mimi nilitaka kumsisitiza acheze na hizi bush kwanza...
Hapo inatakiwa spare ambayo ni OEM.....
Kama injini imetulia gari haina miss...pambana na kwanza na engine na gear box mounts...
 
mkuu unaposema mpya ni za dukani au used? nami zilikata mbili nikanunua mpya dukani kufunga gari ilikuwa inatetema na body nikatoa nikatafuta used za Japan ikatulia.
Mkuu ni USED (Ndio maana nikatumia neon original).
 
Kiongozi...Nina Toyota Voltz WD with automatic transmission, ilikuwa na leakage kwenye mfuniko wa Engine Kwa juu. Fundi ameziba leakage. Baada ya kuziba leakage ameenda kusafisha Kwa kutumia pressure water...From that gari ukiwasha inawasha taa ya check engine...Pia muda mwingine inazima kabisa ikiwa kwenye gia na taa ya check Engine inawaka Msaada Kiongozi. Thanks.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nina kluger ambayo nimeimiliki kwa miezi michache, nina maswali yafuatayo:
(i) Imeandikwa huko nyuma 3.0 FOUR, ina axles 2, je hiyo ina maana ni four wheel drive muda wote?, haina mahali pa kuingizia four wheel drive, japo kwenye utelezi huwa linapita tu bila shida wakati wengine wanapita kwa shida.

(ii) Kwa siku chache zilizopita imeanza tatizo kama ifuatavyo: unapoanza safari na kuweka gia ya D halafu unakanyaga accelerator gari linaondoka kwa shida sana, inakuwa kana kwamba liko kwenye gia ya N, baadaye linaanza kuondoka taratibu sana kana kwamba halina nguvu kabisa lakini likishaondoka linaendelea vizuri tu. Shida inajirudia kama ukisimama, kuliondoa mwanzoni linafanya kama nilivyoeleza hapo juu. Je tatizo ni nini?

(iii) Vifuniko vya nyuma vya fimbo vimeibiwa, nimetafuta sana bila mafanikio, je naweza kuvipata wapi?

(iii) Nikiwasha A/C kioo cha mbele kinapata ukungu inabidi itumie wiper, je hiyo ni kawaida au kuna tatizo la gas kuvuja?
 
Sehemu zipi nzuri na zenye uhakika wa kufanya engine diagnosis, maana mjini hapa kuna kuingizwa mkenge sana.
 
Mkuu mtoa uzi mbona kimya??? Pole kwa kazi na asante kwa kujitoa kushauri watu kuhusu magari hapa. nakuomba uangalie hitaji langu kwenye post #238 na 239. Mimi niko Dar. Ukinielekeza sehemu iliyopo Dar kwa swali langu kwenye post #239 itakuwa vizuri, na nasubiri maelezo yako kuhusu post #238.
 
Za leo kaka,
Samahani kw kmya, pilka kiasi. Kw sasa sina sehemu ni nayo fahamu Dar ninayoweza kuelekezq; mimi mwenyewe hufanya diagnosis na ufundi. Hivi karibuni, ndani ya mwezi huu, nitakua Dar. Twaweza wasiliana kw inbox kupanga

Sent from my Infinix-X600 using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…