Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, tumeingia kwenye Uchaguzi Mkuu mara nne, 1995, 2000, 2005 na 2010 na katika chaguzi zote hizi hakuna uliokuwa na changamoto na wenye msisimko kama wa mwaka 2010. Naweza kusema, ingawa kuna wanaoweza kudai tofauti, kuwa hakuna wakati chama tawala kilijikuta kwwenye hatihati na hofu ya kupigwa chini kama mwaka 2010. Pia kama kuna wakati wananchi kwa ujumla wao walihamasika na kuwa na shauku ya kushiriki katika zoezi hilo, bila shaka yoyote mwaka 2010 hauna mpinzani. Lakini ilikuwakuwaje hadi walioweza kujitokeza kupiga kura wasitimie hata nusu (wakawa pungufu ya asilimia 50%) ya waliojiandikisha?
Lakini linaloleta hofu kuliko hata hayo matokeo ni kukosekana kwa tathmini ya hali kama hiyo ilivyoweza kujitokeza; si Tume ya Uchaguzi, si serikali, si bunge, si vyama vya siasa, si wanaharakati, si wasomi...hakuna kikundi chochote kilichoweza kukaa kujadili, kutafakari na kutoa tathmini ya uchaguzi huo na kutoa sababu kwa nini hali kama hiyo ilijitokeza. Kama kawaida yetu Watanzania inaonekana hakuna mtu, kundi, taasisi wala jumuiya iliyostushwa na hali hiyo na kuhoji kulikoni hivyo leo nimeamua kulileta jambo hili kwenye hili jamvi letu wana JF; tusaidiane kwa mawazo tusiruhusu tena hali hiyo kujirudia huko baadaye tukielekea kutakiwa kupitisha Katiba kwa kura ya maoni.
Kwa mara ya kwanza hebu tujitahidi kutanguliza maslahi ya taifa mbele ya chama, karibuni.
cc: Mchambuzi, Nguruvi3, EMT, Mzee Mwanakijiji, Pasco, Jasusi, JokaKuu, Bongolander, Kobello, Mkandara, Dingswayo, Mimibaba,tpaul, chama, MwanaDiwani, ZeMarcopolo, zomba, Ritz, Pasco, Alinda, steveDii, Kichuguu, Elli, Crashwise, Kitila Mkumbo, Zitto, Mtanganyika, Mr Rocky, Tuko, zumbemkuu, nyabhingi, lynxeffect22, MTAZAMO, Bulldog, Tized, Erythrocyte, MEANDU, jmushi1
| Mwaka | Waliojiandikisha | Waliopiga kura | Asilimia | Kura halali |
| 1995 | 8,928,826 | 6,846,681 | 77% | |
| 2000 | 10,088,484 | 8,517,598 | 84.43% | |
| 2005 | 16,407,318 | 11,365,477 | 72.4% | |
| 2010 | 20,137,303 | 8,397,963 | 42.8% |