Kama ni kesi za jinai ni vigumu kuthibitisha "beyond reasonable doubt" na pia kuna msemo kwamba ni heri kuachia huru wahalifu 99 kuliko kumfunga mwenye haki mmoja. Sheria inamsaidia zaidi mhalifu kuliko upande wa mashtaka na ndiyo maana kesi nyingi za Serikali zinashindwa. Wanasheria ni wale wale na vyuo ni vile vile tofauti ni upande mtu anaofanyia kazi.