Kwa mfano viongozi wa CHADEMA wakikamatwa maandamano yatakuepo?

GenuineMan

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
6,260
Reaction score
14,470
Salaam Wakuu

Sote tunayo taarifa ya mipango ya kufanyika Maandamano. Yanayoandaliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Maandamano hayo yanakuja baada ya vitendo vya utekaji na mauaji ya baadhi ya viongozi wa Chama hicho.

Tayari Jeshi la Polisi Nchini limeshapiga marufuku uwepo wa maandamano hayo. Kutokana na historia ya maandamano nchini hasa hivi karibuni.

Pia soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

Mengi yamekuwa hayafanyiki.
Viongozi wanakamatwa, na hakuna mwanachama anajitokeza barabarani.

Je, kipindi hiki Viongozi wakuu wakikamatwa, kuna mwanachama au mfuasi wa CHADEMA atajitokeza kuandamana au watajifungia ndani?
 
Mambo mengine yanakuzwa tu,
Waachiwe waandamanane,

Viongozi wa Chadema waseme watamtumia barabara zipi, na waahidi ikitokea uharibifu wa mali watawajibika,

Polisi wasimamie na kulinda waandamanaji, wakimaliza watarudi majumbani kwao na maisha yatendelea kawaida,

Wakisubiri ripoti ya mauaji alivyoelekeza Rais,

Hakuna faida kupiga mauaji halafu wanauwawa wengine na kupata ulemavu, busara itumike,
 


Kosa la Mbowe lilianzia pale Tanga.
Leo hii ile jeuri ya chama dume ingekuwa mdebwedo.

lakini pia mbinu za maandamano ni za kitoto sana maana zinadhibitiwa kirahisi sana.

Jiji kama DSm lisilo na mipango miji kushindwa kupanga maandamano ni ufala wa hali ya juu.

Watu laki 5 tu kati ya watu mil. 6 wanatosha kabisa kwenda mpaka Ikulu Kwa Bideni na kutoa mpaka viti nje na kuvikalia lakini kwa sababu wanaopanga maandamano ni wasiotaka maandamano basi hakuna maandamano yatafanyika tarehe 23. Ni kuleta taharuki tu isiyo na matokeo zaidi ya kuua na kubaki na kesi mahakamani kama ile ya Akwiline .

Kule Tunisia walijipanga kwenye Masoko makubwa ndani ya jiji kubwa ,wakafurika masoko ya jirani,wakaanza kuingia soko moja bada ya jingine . Walipojaribu kuwafuata huku wakipita kule wanakimbilia uwanjani ,uwanja ulijaa mamilioni ya watu . Jeshi likazuia Polisi kuua watu mamilioni kwa sababu ya fisadi mmoja. Serikali ni watu hivyo hakuna haja ya kuuana kwa sababu ya serikali ambayo ni watu.
Watu wanatakiwa waheshimiane.

Nimegundua ni kwa nini Kinana aliamua kuachia ngazi. Huenda yale maelekezo ya kuteka na kuua hakukubaliana nayo na waliotoa siri kama akina Nape wanafukuzwa uwaziri na uDC.

Yatayeyuka kama yale ya Ukuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…