Elections 2010 Kwa Mh Mengi na ITV (IPP MEDIA)


Imefika mahali ambapo Bw. Mengi imebidi ameupime upepo uvumao kwa kasi (yaani kasi ya mageuzi)na nafikiri ameshaanza kuhisi moto wa mageuzi unako elekea. Hivyo ameona ni heri ajirudi japo akiwa amechelewa kulikoni kuliko kusubiri historia ije kumhukumu. Hata kama alifanya hivyo kwa kuuza airtime pia tuna mshukuru kwa kutumia hekima na busara zake. Kwani ni heri yake yeye yule ajuaye na akajiepusha na ghadhabu ya Wa-Tanzania kuliko wale wanao endelea kung'ang'ana kuzima kasi ya mageuzi haya ya jayo na kuihujumu demokrasia.

Ni matumaini yangu ITV watatoa Air time zaidi Dr Slaa ili ujumbe wake uzidi kuwafikia mamilioni zaidi ya Wa-Tanzania ambao bado wametawaliwa na hofu ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini na kuweza kukombolewa kwenye utumwa wa CCM.
 
Ndugu zangu miye siku zote nimekuwa nikimchukulia Mengi kama mzalendo wa kweli na mpiganaji. Kwa mtu yeyote wa hadhi yake lazima angekuwa mwoga sana katika kufanya shughuli zake kwani wafanyabiashara wengi nchini hawapendi kwenda kinyume na ccm na kurisk biashara zao. Lakini Mhe. Mengi anapigana kimahesabu sana pamoja na vitisho vikubwa anavyopata tangu wakati anaanzisha kituo chake cha ITV. Wazee si mnakumbuka lile skendo la World Cup 1994 na CTN? Hongera sana Mzee Mengi na dada Joyce Mhavile na timu nzima ya IPP Media kwa uzalendo wenu.

Ombi langu kwenu ni kama walivyosema wenzangu, tunaomba mdahalo wa Dr. Slaa urudiwe tena kwenye 'supper time' yaani baada tu ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Kama ni suala la malipo sisi wananchi tupo tayari kuchanga kwa njia ambayo chadema wataona infaa ili angalau na watanzania wenzetu ambao hawakupata fursa ya kutembelewa na Dr. Slaa, wapate maneno yenye matumaini.

Ndugu yangu, Mzee wangu Mengi umekuwa ukiongelea sana kuhusu ukombozi wa nchi hii tena kwa vitendo. Umekuwa ukitoa misaada kwa wananchi maskini kuliko hata serikali yenye jukumu hilo, kwa ujumla watanzania wengi wanakuchukulia wewe kama Mhe. kuliko hata hao wanaolazimisha tuwaite hivyo. Yote hayo unayafanya katikati ya wafanyabiashara wenzio wanaokumbatiwa na chama cha mafisadi kama akina Patel, Manji, n.k, n.k. Jitihada zako hizo pamoja na wazalendo waliopo Chadema sasa zimetufikisha karibu kabisa na ukombozi wa kweli wa nchi yeti. Ninakuomba sana tena sana ufikirie kwa kina sana ombi letu la kurudia tena mdahalo wa Dr. Slaa na Mungu atakubariki sana.
 
Na mimi naona kuna hja ya kivunjavunja vipande kwenda Oct 31kama wanavyofanya kwenye zile hotuba za nyerere za dakika tatu.
 

katoa bure hayo masaa 3?au ni profit orriented....
 
Ingekua burudani wakiirudia kwa tulioikikosa...
 

Mkuu mimi niko safi na makini, ninachosisitiza ni kuwa Chadema na ccm hawana uwezo wa kumtoa mtu kwenye nyumba ya tembe,huo ndio ukweli hata kama hutaki. pia nilishangaa sana Dr slaa aliposema ndo kaona nyumba ya tembe wakati anafanya kampeini ina maana miaka 15 aliyokuwa anaenda dodoma hakuwahi kuona nyumba ya tembe?????.
Kama maswala ya kuweka mazingira ya kuondoa umaskini vyama vyote vinaongelea hilo. Mwisho ni kwamba vyama vinaongozwa na watu si malaika. Naona wewe ni Mwana Chadema, ukweli ni kwamba Dr Slaa hatafanya maajabu yoyote akiwa Rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…