Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Nina miaka 18 kwenye biashara katika kipindi chote hicho,Nimepitia milima na mabonde.” Yani changamoto” Kitu ambacho ni cha kawaida kwenye biashara yoyote.

Lakini leo nakiri kwamba, Awamu hii imeuwa juhudi za watu wengi kufikia malengo yao kibiashara, Biashara zimeyumba kabisa, Mauzo yameshuka kwa asilimia zaidi ya 70, huku mitaji mingi ya wajasiria mali ikiteketea.

Kinachoogopesha zaidi, Sioni juhudi zozote za makusudi kuokoa hali hii mbaya. Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku.
Lakini tukiwasikiliza viongozi wetu wanasema tupo pazuri. Najiuliza pazuri wapi?

Mwanzoni nilijua labda baba anafanyia nyumba usafi, Cha kushangaza tunamaliza miaka tano hali imekuwa tete zaidi ya tulipo toka.

Kuna hitajika jitihada za ziada kwenye uchumi wetu tena kwa speed kubwa la sivyo tutazalisha taifa la wamachinga na wapiga vibomu. Maana soon kodi za pango na serekali hazitalupika tena.

Natamani hii biashara yangu nimpe bure Dr mpango aiendeshe kwa miezi tu ili ajue hali halisi sio kukaa ofisini huku tukimlipa mshahara mnono bila kusaidia uchumi wetu.

Dr. Mpango mweleze rais hali mtaani ni mbaya,Watu tunapiga kazi asubuhi mpaka jioni lakini tunatoka kapa kila siku.

Halafu nimegundua ukiwa na hali mbaya mfukoni na majukumu ndio yanabisha hodi kwa kasi kweli kweli.

Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.
 
That's why uchumi unayumba these days, serikali imewabana wafanyabiashara wote wakubwa na wadogo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
halafu kwanini upitie mabondeni na milimani.? ina maana huko mjini kwenu hakuna barabara.?
 
Zimbabwe Leo hii Watu zaidi ya milion 5 wanahitania msaada kutokana na uchumi wa taifa lao kuwa duni,lkn Cha kushangaza viongozi wa Zimbabwe wamezidi muwa mabilionea wa mutupwa
Roma mkatolika Zimbabwe inakuja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchumi ni pamoja na uwezo wa watu kununua bidhaa, purchasing power iko taabani mtu anawaambia ati tulieni roli lina mwelekeo.... lishaiona njia.

Mi naanza kujiandaa kuruka hata kama dereva kagoma kupunguza mwendo liwalo na liwe...
 
Wasukuma tuu wanachekelea awamu hii
 
Daaah inafika wakati mtu unataka kufungua biashara lakin unawaza mara mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafanya biashara gani? Ni nini unachoona tofauti na wakati mwingine? eg. kodi imekuwa kubwa, wateja wamepungua etc..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…