Kwa Milioni 200 naweza pata kiwanja cha biashara Morogoro mjini?

Vichekesho

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
66
Reaction score
3,277
Hapa namaanisha kiwanja kilichopimwa, kinachotazama barabara ambayo iko busy mahali ambapo naweza kujenga jengo la biashara na ofisi.

Kiwe na full documents, kisiwe na migogoro, mauziano yafanyike mbele ya mawakili wasomi na wataalamu wa mambo ya ardhi bila kusahau viongozi wa eneo husika.

Je bajeti hii inatosha na kama inatosha ni mitaa gani? ISIWE USWAHILINI
 
Ongeza kidogo.. maana unataka watu wavunje ghorofa zao wakupe eneo
 
Kuna bei elekezi ya thamani ya maeneo mbalimbali nchini kwa sq mita ! Ukiipata itakuwa rahisi kukadiria!
 
Kwa Dar es salaam, pale Manzese au Magomeni kwenye nyumba za uswahilini zinaweza kuuzwa bei gani?
 
Inawezekana mkuu
Morogoro Mimi naiona bado imezubaa
Yaani pale center papo vile vile miaka nenda Rudi
Masika kuelekea msamvu unaweza pata Kwa hela hiyo
 
Unataka wakili wasomi!! Hivi kuna wakili wasio wasomi??
 
Njoo Dm nikuunganishe na Dalali makini! Kama upo serious
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…