Awali ya yote kabla hujaanza kumtafuta huyo mchumba Mshirikishe Mungu kwanza, Hakika Mungu ni Mwaminifu atakupatia aliye ubavu wako sahihi kabisa.Kuhusu uwe na nini nimeona watu wameshakueleza nisingependa kuvirudia tena ila ni lazima uwe na mipango endelevu unapoamua kungia kwenye maisha ya ndoa, usipokuwa na mipango ndoa utaiona chungu,Hiyo sh 10,000 unayoipata lazima uipigie mahesabu na uigawanye sawia na mwisho wa siku upate hela ya kuweka akiba kuna mambo mengi sana siwezi kuyaeleza yote ila ni vema pia ili kuepeuka ugomvi wa mra kwa mara ujue wajibu wako kwa mkeo na yeye ajue wajibu wake kwako mshirikiane kupanga maisha yenu.