Kwa mliofika katika maonyesho ya kibiashara Sabasaba mwaka huu!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari wana Jamii Forums,.

Kwa wale ndugu zetu mliopata wasaa wa kufika katika viwanja vya Sabasaba kwa ajili ya maonyesho tunaomba mtujuze japo kwa uchache kuna jambo gani Jipya limejiri pande hizo.

Maonyesho yaliyopita wanasema yalipoa sana nikimaanisha kulikuwa hakuna bidhaa zinazovutia kama ilivyozoeleka miaka mingi iliyopita nyuma.

Kama umefika tafadhali tufahamise umevutiwa na kitu gani katika maonyesho ya mwaka huu, pia kama kuna Jambo halijakufurahisha tufahamishe pia.

Wengi tupo mikoani tumekosa wasaa wa kufika katika maonyesho lakini naamini Jf ni mahali sahihi tutapata kujua kila kinachojiri pande hizo.


Karibuni,..
 
Kwa kweli nisiseme urongo jana kuanzia saa tano nilikua sabasaba . Nilikagua banda moja tu nalo ni la breweries. kama sikosei nitakua niliondoka pale saa nne au tano usiku. na leo nitalitembelea tena. hivi hayo mengine ni mazuri kama hili la TBL ?
 
Pia watujuze kukoje;

Leo nimesikia kwenye magazeti kuwa
waziri mkuu ameshauri maonesho yasimamishwe
kwa mwaka mmoja ili kutengeneza miundo mbinu.

Je hii imekaa je jamani?
 
Pia watujuze kukoje;

Leo nimesikia kwenye magazeti kuwa
waziri mkuu ameshauri maonesho yasimamishwe
kwa mwaka mmoja ili kutengeneza miundo mbinu.

Je hii imekaa je jamani?

kwani maonyesho uwa yanafanyika mwaka mzima? naona hajafikiria vizuri huyo mkuu
 
kwani maonyesho uwa yanafanyika mwaka mzima? naona hajafikiria vizuri huyo mkuu

Huwa wanakurupuka tu....wakishaziona maiki za waandishi wanachanganyikiwa....na waandishi nao wanakosa ubunifu wa kuwasilisha habari zao....ni janga.
 
Pinda: Sabasaba isifanyike... - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshauri Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Mwalimu Julius Nyerere, maarufu kama Sabasaba, yasimamishwe angalau kwa mwaka mmoja kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ndani ya uwanja huo ili iendane na viwango vinavyostahili.


Pinda alisema hayo jana alipotembelea maonyesho hayo ya kila mwaka yanayoendelea kwenye uwanja huo kukagua mabanda mbalimbali ya kampuni zinazotangaza biashara na taasisi binafsi na serikali zinazotoa huduma mbalimbali.


"Nimemshauri Waziri wa Viwanda na Biashara kuwa viwanja hivi vinahitaji marekebisho. Ongezeko la washiriki wa kimataifa ambao nimeambiwa zimefikia kampuni 500 kutoka nchi 33, inadhihirisha umuhimu na kukua kwa maonyesho yenyewe ambayo sasa nchi mbalimbali zinayazingatia," alisema Pinda.


"Ikibidi tupoteze fursa ya mwaka mmoja ili tuboreshe viwanja hivi tulivyorithi na kuendelea kuvitumia kwa muda mrefu vikiwa na miundombinu ileile. Yatupasa kuboresha kila kitu kwa viwango vya kimataifa. Ukihudhuria maonyesho mengine ya kimataifa katika nchi nyingine unaona tofauti ya ubora wa viwanja vyao ukilinganisha na hivi vyetu… njia ni ndogo na hazijapangwa vizuri."


Mbali na barabara za ndani ya uwanja huo kuwa ndogo, mpangilio mbovu wa mabanda ya maonyesho, umeme kukatika mara kwa mara, uchache wa maliwato na kutokuwapo kwa alama za kuongoza magari yanapoingia hadi kutoka, vimekuwa ni vitu vinavyolalamikiwa sana na washiriki wa maonyesho hayo makubwa kwenye ukanda wa mashariki ya Afrika.


Waziri Mkuu alitembelea mabanda kadhaa na kujionea shughuli zinazofanywa ambapo alivutiwa na ubora unaoonekana katika bidhaa nyingi za kilimo na kupendekeza umakini kidogo uongezwe katika ufungaji wa bidhaa hizo.


"Mnajua kuwa napenda sana asali. Kuna maendeleo makubwa sana nimeyaona kutoka kwa wakulima waliopo kwenye banda la asali… wamejitahidi kuongeza ubora na wanatia moyo kwa kuwa kila mmoja anaweza akaliona hilo miongoni mwa bidhaa zilizopo," alisema Waziri Mkuu na kueleza kuwa changamoto aliyoiona katika vifungashio akiiomba mamlaka husika kuwaongezea uwezo wafugaji wa nyuki.


Pinda aliitaka sekta binafsi kuisaidia Serikali kuboresha huduma za kijamii hasa elimu ya juu baada ya juhudi za Kampuni ya Global Education Link kumfahamisha wanavyoshughulika katika kupeleka wanafunzi nje kufuata taratibu na sheria zilizopo ili wakanufaike na kuja kulitumikia taifa baadaye.


"Juhudi za vijana kama hawa zinapaswa kupongezwa na kuungwa mkono. Wazazi wengi wamekuwa wakipoteza fadha kusomesha watoto wao nje na pale warejeapo wanakataliwa na bodi ya vyuo vikuu lakini kwa namna hawa jamaa wanavyofanya kazi yao kwa uwazi na gharama nafuu. Nashauri vijana wengi zaidi wajitokeze ili kupunguza urasimu uliopo serikalini," alisema Pinda.


"Hakuna taasisi ya serikali inayoweza kukuambia kuwa wanatoa ufadhili kama hawa vijana. Sisi serikali zikiwepo nafasi hizo ni mpaka mtu atafute taarifa, tena kwa shida ndipo azipate."


Kwa jumla, Pinda alipongeza juhudi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) kwa kuboresha na kuyatangaza maonyesho hayo kimataifa kiasi cha kushawishi kampuni nyingi kutoka nchi tofauti kuja kushiriki.


"Maonyesho kama haya yana nafasi nzuri ya kuimarisha uchumi wa nchi kama kampuni ya ndani yatatumia ipasavyo fursa waipatayo kujenga uhusiano mzuri na wenzao wa nje kwa kuwa itawasaidia kujua mahitaji yaliyopo katika nchi mbalimbali waliko na washirika," alisema

kwani maonyesho uwa yanafanyika mwaka mzima? naona hajafikiria vizuri huyo mkuu
 
kwani maonyesho uwa yanafanyika mwaka mzima? naona hajafikiria vizuri huyo mkuu

Bora hata wewe umeliona hilo mkuu, hawa viongozi wetu wana mambo ya ajabu sana kwani kila kitu wao wanataka walete siasa tu!
 
Pia watujuze kukoje;

Leo nimesikia kwenye magazeti kuwa
waziri mkuu ameshauri maonesho yasimamishwe
kwa mwaka mmoja ili kutengeneza miundo mbinu.

Je hii imekaa je jamani?
pinda hata sielewagi akili yake. mbona uwanja unakuwaga wazi miezi 11!?. tukiwasema wanaanza kulia lakini ukichwa maji hauwaishi.
 
Bora hata wewe umeliona hilo mkuu, hawa viongozi wetu wana mambo ya ajabu sana kwani kila kitu wao wanataka walete siasa tu!

eti anasema amemshauri. ye si mkuu wa mawaziri? alitakiwa awaagize.
 
Wakuu kiukweli Saba saba imekosa mvuto, mimi nimekuwapo hapo tangu maonyesho haya yalipoaanza tarehe 28, watu wamechelewa kujenga mabanda yao mpaka jana Mh Seif Khatibu anayafungua maonyesho kwenye ukumbi wa Karume bado kuna watu na nyundo wanagongelea mabanda yao, ughali wa bidhaa, saba saba imekuwa sio maonyesho tena bali sehemu ya kwenda kuuza ni kama watu wanahamishia maduka yao pale kwa muda, mfano box la majani ya chai African tea ninalonunua huku mtaani 2500 hata pale wanauza 2500 hiyo hiyo, wahudhuriaji sio wengi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma........kuhusu miuondo mbinu anayosema Pinda hata mimi namuunga mkono, yale maonyesho hayakidhi viwango vya kimataifa.
 

Mkuu uko sahihi kabisa. Lakini hivi ni kweli wanahitaji kuahirisha hayo maonyesho kwa mwaka mzima ndo wapate fursa ya kurekebisha miundombinu? Kwani yakiisha haya ya sasa hivi si watakuwa na mwaka mzima hapa katikati hadi maonyesho mengine mwakani? Hawa viongozi wetu wafanye kazi waache siasa zao!!
 

Ni kweli hata mimi siungi mkono hilo la kuahirisha maana maonyesho haya yakiisha kuna mwaka mzima mpaka yaje tena, mimi namuunga mkono hapo kwenye yaendane na hadhi ya kimataifa, maana ukifika mfano vyooni hali si nzuri kabisa, kiujumla panahitajika uongozi thabiti kuongoza yale maonyesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…