Kwa mnaopenda kwenda ughaibuni kutafuta Maisha

Kwa mnaopenda kwenda ughaibuni kutafuta Maisha

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,400
Reaction score
14,339
Ndugu zangu kama kawaida yangu Huwa nikipata wasaha wa kuwaasa vijana wenzangu , Huwa sipendi kuwa mchoyo wa taarifa hivyo Leo nimeona niwafunue ubongo maana kupitia bandiko langu nililoweka la fursa za ajira Kwa mnaotaka kuja Dubai, huu ni uzi wenu
Watu wengi wamekuwa wakinitafuta kwaajili ya fursa hiyo ya wao kutoka hapa nyumbani kwenda ughaibuni kutafuta maisha.

Nitaizungumzia Dubai ambayo teyari nimeshaitembelea na ndipo nilipo Hadi sasa.

KWAKWELI KAZI NCHINI DUBAI NI NGUMU 😭😭😭😭

huo ni ukweli ambao ningependa sana ndugu zangu muuelewe hivyo kwa mnaopenda kwenda nchi yoyote ya kiarabu ama nchi nyingine yoyote kaeni mkijua kuwa huko mnakotaka kwenda Kuna upinzani wa watafuta ajira kutoka nchi mbali mbali, huko Kuna Wapakstani, Wasomali, Wahindi WAFILIPINO, Wanaigeria, Wakenya n.k...!

Hivyo nguvu ambayo umeitumia hapa nyumbani kazi Ikawa ngumu kupatikana je ugenini utatumia mbinu Gani kuwashawishi wawaache watu wa mataifa mengine wakuchague wewe...? {Hiki ndicho kikwazo Cha kwanza} 😭😭😭 haswa ukizingatia kuwa elimu yetu Haina thamani kabisa nje ya mipaka ya nchi yetu...

Na kikwazo kikubwa ni kuwa Elimu ya nchi za majirani zetu Ina thamani mno kuliko elimu yetu hivyo vyeti vya elimu zetu ukiacha taaluma za ufundi vyeti vingine vyote SI lolote SI chochote.

Taaluma ambayo kidogo inaweza ikakupa nafasi za kazi Ina weza Ikawa.​
  1. Ufundi nyumba​
  2. Ufundi magari​
  3. Upakaji rangi​
  4. Ufundi wa umeme​
  5. Ufundi umeme wa magari​
  6. Ufundi A/c​
  7. Ufundi bomba​
  8. Upishi​
  9. Customer service​
  10. Ukalimani wa lugha ya nchi unayoitembelea.​
Kongole sana kwa vyuo vyetu vya ufundi stadi {VETA} Hapo mwanzo sikuwa naelewa kabisa umuhimu wa hivi vyuo hizo ni baadhi ya fani ambazo ukiomba kazi huko wanaweza wakakupa nafasi ya kazi ila Bado cheti chako hakitakuwa na thamani kwani thamani ya kazi hizo Haipo kwenye vyeti IPO field 😂😂😂


Kwenye hiyo orodha hapo juu sija itaja fani ya udereva kwa sababu miongoni mwa vitu vigumu na vya gharama sana kupata ughaibuni ni LESENI YA UDEREVA. Kwakweli ili upate kibari Cha kuendesha gari itakugharimu mamilioni ya pesa kwenda shule na kufaulu Kisha ndio upate LESENI.
images (3).jpeg

Na wenzetu awaamini kabisa leseni zetu za kiafrika kwani kule Kuna alama za barabara ambazo huku kwetu hatuna na atujawahi kuzitumia kabisa. Na njia zao zipo tofauti kabisa na tulizo zizoea hivyo dereva yoyote ambae unatamani kwenda nje kufanya kazi ya udereva ukiwa na ndoto hizo sahau kuhusu leseni Yako ya kitanzania 😭😭😭 ni lazima ukasome upya.


Kwa wenye madegree ya fani za ofisini kwa kweli nafasi yenu nchi za mbali ni ngumu mno kwa kuanzia miaka 2 ya mwanzo ni ngumu sana kupata kazi inayoendana na elimu Yako hivyo zingatia orodha ya ajira niliyo itaja.

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA HUJAENDA UGHAIBUNI KUTAFUTA AJIRA.
  1. Hakikisha unapata taarifa sahihi za nchi unayoenda.​
  2. Anae weza kukusaidia kufika kwenye nchi hiyo ni mtu alie po huko na SI vinginevyo.​
  3. Hakikisha Kuna mtu kwenye nchi hiyo anae weza kukupa taarifa za uhakika juu ya nchi hiyo.​
  4. Hakikisha unakuwa na pesa za kutosha hata kama utatumia agent hakikisha wewe mwenyewe unakuwa na pesa zako binafsi.​
  5. Hakikisha ticket Yako ya kurudia ni halali.​
  6. Usiende ukiwa na akili ya kutajirikia ughaibuni ingekuwa kufanya kazi ughaibuni ni UTAJIRI waliopo huko wangerudi na UTAJIRI wa kutosha na wasingekuwa na aja ya kuendelea kubaki ughaibuni.​
  7. Nyumbani ni pazuri sana amini nakwambia Bora uwe mtumwa hapa nyumba kuliko kwenda kutesekea ughaibuni ambako no one will care about you 😭😭😭 kule principal yao ni moja tu minds your business habari za if you scratch my back I will scratch your's kule hakuna😭😭😭​
  8. Hakuna mtu atakupa kipande Cha mkate au kukupunguzia maji 😭😭😭 unaweza ukafa bila kuwaona ndugu zako au kuwaaga tu.​
  9. Siku hizi uki over stay ughaibuni urudishwi kwenu Wala ushitakiwi wanakuacha uwe chokoraa mtaani 😭😭😭​
  10. Ukiwa na bahati unaweza kupata ndugu.​
  11. Ukiwa na bahati unaweza kupata mwenza.​
  12. Ukiwa na bahati unaweza kupata kazi.​
  13. Kwenye kutafuta maisha Kuna kupata na kukosa hivyo malengo Yako yasipo enda kama ulivyo tarajia kurudisha majeshi nyuma sio dhambi {zingatia hili}​

Nikipata wasaha nitarudi ila kwa Leo naomba niishie hapa nakaribisha maswali,​
 
Gulf countries sio za kwenda kutafuta maisha huko nako kuna waganga njaa kama sisi huku.

At least mtu aende Europe au Amerika huko ndiko ughaibuni dunia ya kwanza.
Hakuna nchi rahisi...tusidanganyane...tuweni tu wawadhi watu tuwaambie ukweli wakae wakijua... kuliko kuwapa matumaini hewa...!

Nchi zote ni za kupambania kombe Bora hata Dubai unaweza kujiongeza ukafanya biashara haya huko Europe unafanya biashara Gani...yenye tija😂😂😂​
 
Hakuna nchi rahisi...tusidanganyane...tuweni tu wawadhi watu tuwaambie ukweli wakae wakijua... kuliko kuwapa matumaini hewa...!

Nchi zote ni za kupambania kombe Bora hata Dubai unaweza kujiongeza ukafanya biashara haya huko Europe unafanya biashara Gani...yenye tija😂😂😂​
Kwani kila anayetaka kwenda ughaibuni anataka akafanye biashara?

Huwezi kufananisha Gulf countries na nchi za Europe au Amerika.

Kuna Maelfu ya watu wanatoka Dubai kwenda Europe na Amerika.
 
Kwani kila anayetaka kwenda ughaibuni anataka akafanye biashara?

Huwezi kufananisha Gulf countries na nchi za Europe au Amerika.

Kuna Maelfu ya watu wanatoka Dubai kwenda Europe na Amerika.
SAWA...! Kama umekiri kuwa Kuna maelfu ya watu wanatoka Dubai kwenda huko Europe na American kumbe na kwenyewe sio pepesi...!​
 
Hongera Ila ughaibuni means west countries .

Then Mtaji wa kwanza wa MTU ni kuwa na mtazamo chanya kuhusu MAISHA.

Ikiwa Dubai hapo mnapata ugumu jee MTU utaweza kuishi majiji makuhwa makubwa kama Chicago , Tokyo , wanzuu n.k


All you need is to hold the seed of hustler .



Things are overrated .
 
Ukifa umekufa tu mkuu, mapambano yaendelee lakini kwa akili sana.
Kifo Cha ugenini kinauma imagine unakufa bila kuaga ndugu zako...ama unakufa bila ndugu zako kuwa na taarifa 😂😂😂 na wabongo walivyo masnitch ughaibuni awakusaidii mpaka waone unakata roho... Joks kwa Dubai huwezi kufa Kuna umoja wa watanzania wenye upendo sana​
 
Back
Top Bottom