Kwa mnaopenda kwenda ughaibuni kutafuta Maisha

Kuishi inawezekana ila kwa mchongo maalum nilicho jaribu kufanya ni kuwapa watanzania picha ya nje ya kile wanacho kitafuta ili Kila mmoja aamue ayavulie maji nguo au alale bila kuoga...!

Unajua Bora upambane na adui unae mfahamu kuliko kupambana na adui ambae hujui anafananiaje...!​
 
Narudia tena ukifa umekufa hata ukiwaaga haisaidii chochote mkuu.
 
Asante kwa kuwa muwazi na Mimi naomba niongezee kwa wale ambao mnataka kwenda ughaibuni muangalieni huyu dada YouTube channel Official Dating Assistance anatoa madini sana kwa kuhoji watu wanaoishi huko..

La mwisho bro punguza matumizi ya emoji unawapa green light mabazazi.
 
Acha basi mwanangu
 
kauli ya kishujaa sana hii mkuu utatoboa haraka sana kama utaweza kusimamia msimamo huu
 
Kuna mwamba alifungua uzi unashbihiana wako titled "wanaotaka-kuzamia-ughaibuni-fursa-tele-gaza-syria-na-ukraine"
Natamani hizi nyuzi ziunganishwe!
Hongerani sana Wakuu kwa kuwajali wabongo wenzenu.

However, Nina maoni haya kuhusu fursa za Kimataifa ikiwemo Middle East!

UNRWA ambaye ni mwajiri mkuu katika ukanda huo imepigwa pini na Israel. Hivyo yameibuka mashirika mbalimbali mapya ya kutoa misaada East Bank na Ukanda wa Gaza. Aidha, vijana wengi wakipalestina waliokuwa wanafanya kazi husika wamepoteza maisha hali iliyofanya kuwepo na uhaba wa rasimali watu. Pia, mashirika mengi ya kimataifa yanasita kuajiri vijana wa kipalestina kutokana tension ilivyo ktk eneo hilo.

Kwa hali hiyo vijana wenye kumudu kuongea English na Kiarabu wana fursa ya kuajiriwa huko. Hii ni fursa kwa wauguzi, madktari, vijana wa veta, wajenzi, walimu hasa sayansi, mathematics na psychology, walinzi wakiwemo mgambo, polisi na wanajeshi, wajenzi n.k
Mara nyingi mshahara unategemea na uzoefu na aina ya kazi ila minimum ni around USD 2500 - 7000 kwa local positions na USD 6000 - 13,000 kwa professional staff kwa mwezi. Ukichanganya na posho mbalimbali kipato kwa mwezi kinaweza kuongezeka hadi USD 25,000 ikitegemea na ngazi ya cheo.
Note: risk ni kubwa; lakini penye nyuki, wakali ndipo penye asari nzuri. Na nirahisi kupata fursa maeneo yenye risk kubwa hasa vita.
Nasisitiza mtazania yeyote ambaye amefanya mafunzo ya kijeshi na ana cheti na uzoefu wa kazi pamoja na kumudu kuongea kiingereza na kutokuwa na kitambi ana fursa kubwa ya kupata ajira za kimataifa. Njagu Changamkieni fursa!
Mnaweza kuchungulia hapa:
Jobs at UNOPS
https://unjobs.org/duty_stations
https://unjobs.org/duty_stations/gza
https://unjobs.org/organizations
Vacancies
UNDP Jobs
https://unhcr.wd3.myworkdayjobs.com/External
UN Careers

Search | International Committee of the Red Cross
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…