MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Tangu hilo gari lizame na huyo mama, kuna Watanzania wamekua wakibeza sana kama kwamba wanashangilia tukio na ingekua furaha sana kwao kama juhudi za uopoaji zingeshindwa kufaulu, roho nyeusi kupita maelezo, wao wamesahau huko kwao kipindi cha mkasa wa MV Nyerere kuna watu wangeokolewa ila kwa ukosefu wa taa usiku, ilibidi waachwe wafe tu ili miili yao iopolewe, na pia haikuopolewa yote, kunao wengi waliachwa waliwe na samaki.
Inategemea uwezo wa kutumia ubongo na kudadisi huu mkasa wa Kilifi ulikuwa kwenye mazingira gani, kina cha mita 50 na mzunguko mrefu wa mraba, ukizingatia hayo maji yana kitu tunaita 'rapid under current', hiyo ina maana gari halikuzama moja moja kwenda chini, lilisafirishwa humo humo ndani na kupelekwa mbali, pia kuna kitu kinaitwa 'zero visibility', ilibidi watumie special vision equipment maana kwa macho ya kawaida hauwezi kuona kitu.
Nguvu na gharama nyingi zilitumika kuopoa maiti ya huyo mama, ni faraja kuona serikali yetu inaweza kwenda hatua zote hizo kuopoa maiti ya Mkenya mmoja.
Japo pia maswali yanafaa yapate majibu ili kubaini uzembe uliosababisha huo mkasa.