Kwa mtaji huu stars hashindi hata mechi moja

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Hivi hakuna cha kulitangaza jina la Tanzania bali jina la Rais?

Kuna vitu kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Madini Tanzanite na hata Fukwe zetu na sio Magufuli.

Hivi akili zetu zimefikia hapo kweli? Utaweza kuona jezi zimeandikwa Kenyatta au Museveni huko Misri kweli?

Kujipendekeza huku kwa TFF kuna zidi kabisa kujipendekeza kwa Kabudi.

Kwa ujinga huu Stars ataondoka bila point hata moja Misri. Uzi huu mtaukumbuka.

 
Muda wa kula huu na miiko wakati wa kula hutakiwi kuongea
 
Sijaelewa[emoji848][emoji848][emoji848]
Jezi watakazochezea stars zmeandkwa hvyo?
This aint serious
 
Ngoja ni weke siti hapa. Nitarudi baada ya AFCON InshaAllah
 
Labda ni mfano...
vinginenvyo ndiyo maana wasaidizi hawa wanatukanwa, wanaitwa WAPUMBAVU.... Kwa akili hii utasema tuna great thinkers kweli kama Taifa?
Tatizo la kutojitambua na kuokotwa majalalani.... Kama itakuwa hivyo, Mungu waadhibu Watanzania kwa dhihaka juu yako. Wanajikweza sana, uongo mwingi!
 
Kama ni hivyo basi ninasitisha safari yangu ya Cairo kwa kuwa tumeshashindwa kabla ya mashindano hayajaanza!
 
Mkuu hapo mbona hamna shida hata kidogo au thinking capacity ndiyo tatizo. Kilichozinduliwa ni jezi mpya hilo jina Magufuli hapo nyuma limewakilisha jina la mchezaji yaani wangeweka jina lolote kuwakilisha majina ya wachezaji siyo kwamba jezi zote zitakuwa na jina la Magufuli. Mfano kipa wetu ni Aishi manula jezi yake litakuwa na jina la Aishi manula lakini litaandikwa kwa mfumo huo wa hilo jezi lililoshikiliwa hapo . Kwa maneno machache hiyo ni SAMPLE tu wangeandika hata jina la MAKONDA AU MAALIM SEIF haingemaanisha ni hivyo kwa jezi zote. Si kila jambo la kupinga hata kama hujaelewa bwana mkubwa kuuliza ni muhimu. Halafu usidhani jezi ziko 23 tu ziko nyingi na hata wewe unaweza ukawana original jezi yenye jina lako.
 
Dah...Msaada...aliyesoma na kuelewa ..kuanzia mwanzo hadi hapa...naomba anieleweshe ...bure tu
😎
 

RC Makonda anataka sana kuwa Mbunge katika moja ya Jimbo la Mkoa wa Dar es Salaam na hasa hasa la Kawe lakini pia RC Makonda ameshaaminishwa kuwa anakuja kuwa Rais wa Tanzania hivyo tayari ameshasoma Saikolojia ya Watanzania hasa kwa wana Dar es Salaam kuwa wanapenda Mpira na tayari ameshamuweza Rais wa TFF Karia hivyo Karia anatumika Kufanikisha lengo lake hilo ambalo kwa mtazamo wangu tayari naona kama vile RC Makonda ameshalifanikisha. Ipo Siku hata Ofisi za TFF zote zitahamia hapo Ilala Boma zilipo Ofisi za Mkuu wa Mkoa Makonda na Timu ya Taifa itachaguliwa na Makonda pia.
 
Ni matakwa ya Naibu Rais. Naye kwenye zile za njano kaandika jina lake “MAKONDA”.
 
Kuna haja gani ya kuonyesha jezi ya Magufuli kwa vyombo vya habari na si ya Samatta?

Hawajui kuna majina yanatia watu hasira au..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…