Kwa mtaji huu uchumi utaimarika

Nsera Ndawani

Senior Member
Joined
May 5, 2013
Posts
136
Reaction score
38
​serikali yetu inaruhusu kucha bandia, nywele bandia, tooth pick, midoli ya bunduki, magari kuukuu, kuingizwa nchini kwa kutumia pesa kidogo za kigeni zinazopatikana kwa kuuza pamba nje. Na pia inauza magogo kwa bei ya kutupa na baadaye kwenda kununua tooth pick kwa bei kubwa zinazotokana na uchafu uliyotolewa kwenye gogo, mali asili zetu ikiwemo madini,nayo yakigawiwa wageni bure. Jee kwa mtaji huu tunaweza kukua kiuchumi?
 
Topic nimeielewa
maelezo nimeyaelewa
swali nimelielewa
sasa hayo maelezo Yanacompliment topic au swali
 
NIMEJARIBU KUTOA MAELEZO KIDOGO KUWA HAYA YAKIENDELEA KUFANYIKA YANAWEZA KUFANYA UCHUMI WETU UKUWE? swali
Topic nimeielewa
maelezo nimeyaelewa
swali nimelielewa
sasa hayo maelezo Yanacompliment topic au swali
 
Kwa mtazamo wako unaona hii serikali ya awamu ya nne ina nia thabiti ya kukabiliana na uchumi? Pia kumbuka hizo hela za kigeni zinazotokana na pamba, madini na magogo zimekuwa hazitoshi na serikali akaamua kukopa na deni sasa limefika 22 trillion serikali ikiamini ndo njia mbadala kukopa kuliko kutumia ipasavyo rasilimali zetu
 
Uchumi kukua zitabaki kuwa ndoto tu na hadithi za kufikirika maana wenye dhamana ya kutunga sheria na sera+ watendaji na wasimamizi wote hawana hata wazo la kukuza uchumi wa nchi kila mtu anawaza familia pamoja na tumbo lake mwenyewe yuko radhi kutupa bilions za pesa za serekali kisa apate milioni mia za kwake,hii ndo Tanzania yetu sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…