Kwa mtaji wa elfu 20 naweza fanya biashara gani?

Mtaji kwa elfu 20
-Mchicha
-Karanga
-Vitabu vya nursery kutembeza
-Vocha
-Maji
-Chai....
 
Fanya biashara hii mavyuoni, sehemu za wateja uwe unazunguka kwenye vimbweta wanavyotumia wanafunzi kujadiliana na kufundishana/

Nunua rim yenye karatasi 500 kwa elf nane.
bana karatasi nne nne uwe unauza kwa 200
hapa faida kwa rim moja ni elf 17

nunua boksi la peni za obama kwa elf 5 uwe unauza moja kwa 200
faida kwa boksi ni elf 5

Cha kufanya uwe unatembea na begi lako lenye rim na peni huku ukiwa mkononi ukiwa na karatasi chache na peni chache, siri ya hii biashara ni uvumilivu wa wiki moja tu ili wanafunzi wajue kwamba wakitaka karatasi zilizobanwa au peni wakutafute wewe. ukishazoeleka ndani ya muda mfupi nakwambia utaanza kuzoeleka na unaweza kuanza kuuza rimu nzima na boksi lote la peni ndani ya siku.
 
Hakuna biashara ya mtaji huo kwa sasa utajichelewesha tu fanya saidia fundi uongeze mtaji
 
mkuu ongeza kidogo hiyo pesa ifike 30,njoo nikupe mchongo wa kutengeneza sabuni za maji. nitakusaidia kutengeneza, kisha ukiwauzia wakinamama,faida ni Mara 2,ya pesa yako.asante kwa maelezo zaid.,..........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…