Mkuu
chembamba
Unaweza kufanya hivi na hiyo Million 2.5 yako, Toa laki 6 nunua guta (yanauzwa pale kikituo cha tazara kwa mbele yaani unajipatia guta jipyaaaa) then mtafute mwaminifu akuletee pesa kwa wiki 30,000.
Pesa inayobaki ni kama Mil 1.9 ingia nayo mzigoni Njombeeee fata Kiazi CAP. Hapo anza na gunia 20 kwanza, mzigo ukisha fika town unajikusanyia order kutoka kwa wateja zako then Kwa kutumia lile guta lako wasambazie kiazi wateja zako ambapo watalipia gharama ya usafiri wa guta kutoka store kwako hadi site kwao.
Ok, tupige mahesabu Guta 30,000 kwa wiki kwa mwezi ni 120,000. Then jitahidi upige tripu nne kwa mwezi ulete kiazi na hakikisha kila gunia faida yako ni 20,000 (Hii ni faida naipendekeza mimi ingawaje unaweza kuongeza zaidi ila hii itakusaidia kuuza mzigo fasta na kujipatia wateja zaidi) ambapo 20,000 kwa kila gunia kwa gunia 20 ni laki 4 ukipiga mara 4 (kwa mwezi 1) ni kama Mil 1.6 jumlisha na hesabu ya 120,000 jumla ni Mil 1 laki 7 na elfu 20 (1,720,000).
Sasa mkuu usilale komaa kwelikweli kiuanaume ndani ya miezi 6 utakuwa na si chini ya Mil 8 kwenye account yako, hiyo ni faida tu jumlisha na mtaji wako Mil 1.9 Jumla utakuwa na si chini ya Million 10.
Sasa Piga mara kumi..................Aaaaaaaaaghhhkkkk Mpwa naumia kukuona JF unatangatanga wakati umeshikilia utajiri wako mwenyewe Damnnn,,,!